Watanzania wenzetu,
Tunapenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu kwamba Jumamosi inayokuja (i.e. September 28th, 2013) kutakuwa na ufunguzi wa tawi la CCM Ohio kuanzia saa kumi kamili jioni.
Mgeni rasmi katika ufunguzi huu atakuwa Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania.
Hii ni nafasi ya sisi wote kama Watanzania, sio lazima uwe mwanachama wa CCM au chama chcochote cha siasa ,kupata fursa ya kukutana na watanzania wenzako kutoka miji mbalimbali ya Ohio na Kiongozi/Viongozi wa nchi yetu.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na
Fredd Mujuni - Mwenyeketi : 216- 225-1585
Joe Ngwilizi Muhaya - Katibu Mkuu - 330-685-8625
NB: Maelezo ya jina na anwani ya ukumbi yatafata siku chache zinazokuja
Ahsanteni,
Mungu Ibariki Tanzania
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...