Kesho jumapili 22.9.2013 kuanzia saa nne asubuhi pale kwenye hotel ya Lamada Hotel & Apartments, kutakuwepo na usaili ( auditions) kwa ajili ya shindano jipya la Tanzania Top Model linalotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu hapa hapa Dar es salaam. Usaili huu utakuwa ni mwendelezo wa usaili uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika miji ya Mwanza, Musoma na Sirari ambapo wanatafutwa wanamitindo 20 watakao jiunga na kambi ya taifa ya Tanzania Top Model.
Tunatoa mwito kwa Wanamitindo wa mikoa ya Morogoro, Pwani, Lindi,Mtwara na Dar es salaam kujitokeza kwa wingi kwenye usaili huu ili waweze kupata nafasi ya kushiriki na ikiwezekana kushinda taji la Tanzania Top Model na kuwakilisha nchi yetu kwenye mashindano ya Top Model of the World mwakani.
Washiriki watakaobahatika kuchaguliwa na kujiunga na kambi ya Tanzania Top Model ambayo itakuwa ni tamthilia halisi ya kwenye Luninga, watafundishwa mambo mbali mbali na kutafutiwa mikataba.
Imetolewa na
Jackson Kalikumtima
Mwenyekiti mtendaji
American next top model,na sie tuna ya kwetu Tanzania top model,big up TANZANIA
ReplyDelete