Tamasha la Mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za asili nchini Saida Karoli limefana usiku huu kwenye ukumbi wa Lina's Night Club Bukoba. Tamasha lililokuwa linaitwa "usiku wa Saida Kaoli" ambalo  watu wengi wakijitokeza kumuona kwa mara nyingine hapa Bukoba Tangu azushiwe na wadau kwamba alifariki Dunia katika ajali ya boti miezi michache iliyopita.Saida kajitokeza kuthibitisha kuwa  habari hiyo ilikuwa ya uzushi mtupu na ya uongo. Leo hii Jumamosi akiwa amesindikizwa na wasanii wa  Nyumbani kwao Bukoba Bk Sande, Papaa Kishaju, pamoja na wanamuziki wa VISION MUSIC AMBASSADOR wanaodhaminiwa na 100.0 Vision fm Radio BUKOBA na Kundi la Ka Jay Poda kutoka Kenya amabo wameusindikiza usiku wa SAIDA KAROLI vilivyo na kukamua kisawasawa.
Saida Karoli akiimba baadhi ya nyimbo zake mpya
Willy Kiroyera kulia akicheza na Saida Karoli

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AFUNIKAGE TUMBO

    ReplyDelete
  2. Sawa kabisa, afunike tumbo pia ajifunike mpaka kwenye maeneo ya magoti.

    ReplyDelete
  3. Hivi wanamusic kama huyu wanakuaga wapi? Wazazi wake,maana kwajinsi alivyo vaa mpaka naona kichefuchefu,nahuu mtandao wa kijinsia uko wapi? Why wasiwapige malfuku kwa Uvaaji huu unaozalilisha akina MAMA zetu na MADADA zetu hii ni aibu kubwa kwa kitaifa,amakweli mambo ya utandawazi ni hatali kubwa,kwa mwendo huu TANZANIA Ukimwi kwisha itakua NDOTO za Alinacha,mungu waepushe Madada zangu woote wakitz

    ReplyDelete
  4. MSISHANGAE SANA, ANAONYESHA ALIKOTOKA

    ReplyDelete
  5. Jamani dada funika tumbo lako basi!

    ReplyDelete
  6. Dad Saida ina maana pesa umepata zimekupoteza, zamani ulikua unavaa vizuri watu akakupenda sasa tena nini? Hivi savi umekua si mtoto tena umri umesogea imba lakini jisitiri vaa vizuri utapendeza tuu sio kuacha mwili wazi kama hivyo aibu kwa wanawake wote unatuaibisha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...