Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe Batilda S. Burian,  leo ameongoza umati wa Watanzania waishio hapa Nairobi, Kenya,  kujitolea damu kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tukio la ugaidi lililotokea Tarehe 21 Septemba 2013 jijini Nairobi Kenya, ambapo hadi sasa zaidi ya watu 62 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 179 wamejeruhiwa vibaya na wengi wao bado wanaendelea kupata matibabu katika hospitali za Aga Khan University Hospital, Hospitali ya Nairobi ( Nairobi Hospital), na Hospitali ya MP Shah.

Katika tukio hilo pia Mtanzania, Bwana Vedastus Nsanzungwanko, Meneja, Child Protection, UNICEF ni mmoja wa wale walioathirika na tukio hilo ambapo alijeruhiwa kwa risasi na magruneti katika miguu yake yote miwili. Hivi sasa Bwana Vedastus amelazwa katika hospitali ya Aga Khan, Nairobi na anendelea kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
Mh. Balozi Batilda S. Burian akiwa katika zoezi la kutolewa damu pamoja na watanzania wengine aliyoambatana nao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...