•       Wateja wanaweza kuhamisha pesa  kutoka kwenye akaunti zao za benki

kwenda kwenye akaunti ya Airtel money masaa 24 siku 7 za wiki.
•       Ni njia salama, rahisi ya kupata pesa kupitia kutoka Airtel



Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel money imeanzisha ushirikiano na benki mbalimbali nchini na kuwawezesha wateja wake kuhamisha pesa kutoka kwenye benki akaunti zao na kuziweka kwenye akaunti ya Airtel money. Benki ambazo zimeingia katika ushirikiano huo na Airtel ni pamoja na Tanzania Postal Bank, Bank of Africa, Kenya Commercial Bank, Barclays Bank, Akiba Commercial Bank, Exim Bank, Amana Bank, Mkombozi Commercial Bank na Standard Chartered bank.

Akiongea juu ya ushirikiano huo Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi. Beatrice Singano Mallya (pichani) alisema” kuanzishwa kwa mpango huu wa huduma ya Airtel money na za kibenki kutawawezesha wateja Airtel kutoa pesa kwenye akaunti zao za benki na kuziweka kwenye simu zao yani akaunti ya Airtel money kirahisi bila kutembelea ofisi za benki.  Huduma ya Airtel Money ni suluhisho la huduma za kifedha ikiwa na zaidi ya mawakala 20,000 , kupitia mtandao wetu mpana ulioeneea nchi nzima tunauhakika wa kuwafikia watu wengi zaidi hasa wa maeneo ya vijijini”



Tunaamini ushirikiano na benki zingine kutaendelea kuwaletea wateja wa huduma ya Airtel money ufanisi na urahisi wa upatikanaji wa fedha kutoka kwenye benki zao wakati wote mahali popote nchi nzima.”

Mallya aliendelea kusema Airtel imedhamiria kutoa huduma za kiubunifu kwa watanzania kwani tunatambua tecknologia ya simu inazidi kukua na kuunganisha watu na kubadili maisha ya jamii.  Huduma ya Airtel money
inatoa mwanya kwa makampuni, watoaji huduma za kitechnologia inawezesha huduma za malipo na kukuza huduma za kifedha nchini. Airtel imejipanga kutoa huduma za kifedha na kuiwezesha kuwa ya mafanikio
aliongeza Mallya.
Akiongea kuhusu ushirikiano meneja huduma wa Airtel Money Bw , Asupya Nalingingwa Alisema” tunafuraha kuingia kwenye makubaliano haya ya ushirikiano wa kutoa huduma za kifedha na benki hizi tofauti ambapo
kwetu ni nafasi nzuri ya kuendelea kuboresha huduma za kifedha nchini na kuwafikia wateja wa benk hizi na wateja wa Airtel wasio na huduma ya benki hizo maeneo ya karibu.
Ili kupata orodha ya huduma za benki husika mteja anatakiwa kupiga namba zifuatazo na kufuata maelezo Tanzania Postal Bank –*150*21#, Bank of Africa –*150*13#, Kenya Commercial Bank –*150*22#, Barclays
Bank –*150*20#, Akiba Commercial Bank –*150*10#, Exim Bank –*150*11#, Amana Bank –*150*12#, Mkombozi Commercial Bank –*150*06# , Standard Chartered Bank – *150*65#
Huduma ya Airtel money inawawezesha wateja kulipia bili zao, kutuma na kupokea pesa na kufanya miamala mbalimbali, huduma hii inapatikana kwa wateja wa malipo ya awali na ya kabla , kujiunga na huduma hii ni bure kwa kupita maduka ya Airtel na mawakala nchi nzima.  Mpaka sasa Airtel Money  inamawakala zaidi ya 20,000 Wanaotoa huduma za kifedha kwa wateja nchini. Airtel inatoa huduma ya Airtel money kwa msharika na watu binafsi kama njia mbadala ya malipo.


Airtel pia kupitia Airtel Money kwa sasa imezindua promosheni mpya ya Hakatwi mtu hapa  inayowawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bila makato yoyote popote pale nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. NMB,NBC na CRDB mbona hazipo?

    ReplyDelete
  2. Zaidi ya Huduma za Kibenki kwa njia ya Airtel, masuala ya Kifedha ndio Ubosi wenyewe !!!

    Ubosi mwingine kwa wengi wetu wa Watanzania ni hiyo POSTING YA CHINI HAPO ILIYOTANGULIA HII.

    NI KUWA BIDHAA HIYO YA DAWA YA KUKATA KITAMBI ITAPATA CHANGAMOTO KWENYE MASOKO KWA KUWA KWA WATANZANIA WENGI SUALA LA KITAMBI NI ZAIDI YA KITAMBI NI KUWA, KITAMBI NI:

    1.KITAMBI NI MTAJI:
    Wengi hufuga Vitambi ilium kuweza kukubaliwa wanapo Kukopa wanapo chacha.

    2.KITAMBI NI UJIKO:
    Wengi wa Watanzania Kitambi kwao ndio afya na ujiko kuwa mtu ni Bosi!!!

    3.KITAMBI NDIO HESHIMA:
    Inaweza kutokea ukafika sehemu halafu mapokezi yakazingatia ukubwa wa Kitambi cha muhusika, ukiambatana na mtu mwenye 'mimba' kuwa itabidi kukabiliana na uyamudu majaribu ni wazi ya kuwa mwenzako ndiye atakaye pewa kipaumbele kwenye kukaribishwa inawezekana wewe usipatiwe kiti cha kukaa lakini bonge nyanya akapewa kiti kwa haraka zaidi!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...