Waziri wa Ujenzi Mh. Dkt. John Magufuli (kushoto) akiongea na Waziri wa Uchukuzi wa Malawi Mh. Sidik Mia(kulia) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam(katikati) ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Hebert Mrango.
Waziri waUjenzi Mh. Dkt. john Magufuli (kushoto) akimkabidhi nyaraka Waziri wa Uchukuzi wa Malawi Mh. Sidik Mia (kulia) leo jinini Dar es Salaam,walipokutana na kuzungumza masuala mbalimbali yakiwemo kuimarisha ushirikiano katika nyaja za usafirishaji .(katikati) Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Hebert Mrango.
Waziri wa Ujenzi Mh. Dkt. John Magufuli (kushoto) akiaagana na Waziri wa Usafirishaji kutoka Malawi (kulia) Mh. Sidik Mia pamoja na baadhi ya ujumbe wake baada ya kumtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam,(katikati mwenye tai nyekundu) ni Waziri wa Nishati wa Malawi Mh. Ibrahim Matola. Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Huu ni wakati muafaka wa kuimarisha uhusiano na majirani waliotayari. Kuimarisha kikwelikweli na kuwaepuka, kujihadhari na kujilinda dhidi ya wapenda vita.

    sesophy

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nikweli ulivyo andika lakini ukumbuke serikali zetu za kiafrika zimezidi uchoyo na ubinafsi, ndiomaana mikwaruzano haikosi kila kukicha. Angalia nchi za kiarabu wanavyo teseka leo hii na utajiri wao wa mafuta, inamaana kungekuwa na utawala wa haki hata sisi wa pembeni tungenufaika na amani za majirani, lakini kwa uchoyo na ubinafsi wa tawala zetu huko Afrika ndio chanzo cha migogoro na umasikini. Sisi tulieko nje ya TZ tunayaona na ndio maana tumeamuwa kuishia kuwa watumwa kwenye nchi za wazungu kwakuwa haki ni kwa yeyote mwenye uhai hata PANZI wa ulaya unahaki ya kuishi bila karaha. Hiyo migogoro haiwezi kuisha bila viongozi wetu kubadilika na kujuwa kuwa wote tunahaki ya kuishi popote duniani. Leo hii Tanzania inafukuza binaadamu katika ardhi eti ni wahamiaji haramu, swali ni jee hao wahamiaji haramu wmekuishi miaka zaidi ya ishirini wameowa na wengine kuolewa na kuzaliana wewe unaewaita haramu ulikuwa wapi mda huo? Jamani waafrika tubadilike tupendane maana aridhi hiyo ni yetu sote ningeomba tuvumiliane kwani sote tunapita tuu, kwani ni mda wa miaka 75 ys unaondoka na wengine wanaendelea. Tuache uchoyo

      Delete
  2. Kizi bado ipo kwa waziri wa uchukuzi kuhusu kilio chetu cha upimaji wa mabasi ya abiria kwenye vituo vya mizani kila sehemu imekuwa kero kwa abiria, tunaomba sababu ya msingi kupima basi, kwani uzito ukizidi inakuweje? Na kama mizani ni chombo cha kudhibiti uharibifu wa barabara jeee kutoza faini waliozidisha uzito na kuwaruhusu waendelee na safari kunasaidiaje udhibiti na hali uzito umeendelea na safari? Mimi ningeomba faini isiwpo isipokuwa mzigo uliozidi ushushwe usiende kuharibu na huko mbele kwani faini haisaidii kuimarisha barabara. Hata basi likizidisha uzani basi abiria wapunguwe, na kama basi halijawahi kuzidisha uzito kwenye vituo vya mizani basi tunaomba hiyo sheria ya kuingiza mabasi ya abiria kwenye mizani iondolewe kwani imekuwa keroooo haswa mizani ya Kibaha na Dodoma

    ReplyDelete
  3. Tutaongea mengi lakini ni muhimu Malawi waelezwe waziwazi ya kuwa Ziwa looote hawapati ng'o, !

    La muhimu ktk Ziwa Nyasa Tanzania ina maji na sehemu yake ya ziwa na Malawi ina maji na sehemu yake ya ziwa.

    Hivyo misafara mingi kuja Tanzania na kuweka vikao haitasaidia kitu!!!

    ReplyDelete
  4. Waziri wa Uchukuzi wa Malawi ukifika kwenu kamweleze Raisi wako Joyce Banda ya kuwa alipokaa na Raisi Kikwete na Waziri Membe aligonga mwamba na ukuta Ziwa hakulipata!

    Na kuwa hata yeye Waziri wa Uchukuzi alipotumwa na Joyce Banda kuonana na Waziri Magufuli akakutana na kizingiti kingine JOHN POMBE MAGUFULI akiwa mkali kama Kikwete na Membe!

    Hivyo ziwa amelikosa tena!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...