Meneja Airtel Mara Joseph Mushi (kulia) akimkabidhi makamu mkuu wa
shule sekondari Kasoma (kushoto) bw, Mtaki Bita msaada wa vitabu
vyenye thamani ya milioni 5 vilivyotolewa na Airtel kwa shule ya
sekondari ya kasoma iliyopo Majita wilayani Musoma mkoani mara ambapo
Airtel imetoa msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi katika masomo ya
kemia, fizikia, baiolojia na hisabati.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea na kampeni yake ya
kusaidia elimu hapa nchini kupitia mpango wake ujulikanao kama shule
yetu.
Msaada huo umetolewa katika shule ya sekondari ya Kasoma ilipo Majita
wilayani Musoma mkoani Mara ambapo Airtel imetoa msaada wa vitabu vya
masomo ya sayansi.
Afisa masoko wa Airtel kanda ya Ziwa Bw. Ally Mashauri amesema, msaada
huo unakuja ikiwa ni kuitikia wito wa serikali wa kusaidia katika
masomo ya sayansi nchini.
Afisa Masoko airtel kanda ya ziwa Ally Mashauri alisema “ Airtel
inatambua kuwepo kwa uhaba wa vitabu na vifaa vya kufundishia katika
shule zetu na katika kutatua changamoto hizo tunaongeza nguvu na
kushirikiana na Serikali chini ya wizara ya elimu kuweza kuinua sekta
ya elimu.
Nae Joseph Mushi ni Meneja wa Airtel mkoani mara anaelezea umuhimu wa
msaada huo huku makamu mkuu wa shule ya kasoma Mtaki Bita akishukuru
kwa msaada huo.
“huu ni msaana sana katika kuoneza hari ya waalimu kufundisha masomo
ya mchepuo wa sayansi na pia wanafunzi mkoa huu wa Mara kupenda
kusomea sayansi kwa kuwa nyenzo za kusomea zimepatikana” alieleza
Joseph Mushi meneja airtel Mara
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa shule kasoma sekondari Mtaki Bita
alisema Ninawashukuru sana Airtel kwa kuchangia elimu katika mkoa
wetu, lakini bado ninawapa taarifa Airtel na wadau wengine wote kuwa
bado shule yetu inachangamoto nyingi sana ambazo bado zinahitaji
msaada wa wadau wa elimu ili tuijenge Tanzania yetu”.
Msaada uliotolewa unahusisha masomo ya kemia, fizikia, baiolojia na hisabati.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali
ikiwemo ukarabati wa shule, sare za shule, kompyuta pamoja na
kuunganisha baadhi ya shule kwenye mtandao wa internet wa Airtel wa
3.75G ili kurahisisha wanafunzi kujisomea kupitia mtandao.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...