Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha na Balozi wa Marekani nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Mhe Alfonso Lenhardt na mke wake leo walipofika Ikulu kuaga na kumshukuru Rais na serikali yake kwa ushirikiano alioupata katika kipindi chake cha ubalozi hapa nchini.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuaga mke wa Balozi wa Marekani nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Mhe Alfonso Lenhardt leo walipofika Ikulu kuaga na kumshukuru Rais na serikali yake kwa ushirikiano alioupata katika kipindi chake cha ubalozi hapa nchini. Mama Salma Kikwete alikuwepo pia katika kuwaaga wanadiplomasia hawa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Balozi wa Marekani nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Mhe Alfonso Lenhardt leo walipofika Ikulu kuaga na kumshukuru Rais na serikali yake kwa ushirikiano alioupata katika kipindi chake cha ubalozi hapa nchini.PICHA NA IKULU.
========= ====== =======
Balozi wa Marekani amaliza muda wake hapa Nchini
Tanzania na Marekani zimeimarisha mahusiano yao katika kipindi cha miaka minne iliyopita kutokana na uhusiano na ushirikiano mzuri wa balozi anaemaliza muda wake nchini Mh. Alfonso Lenhardt.
“Asante kwa kazi nzuri uliyoifanya katika kipindi chote cha miaka minne uliyoitumikia hapa Tanzania. Mambo mengi na makubwa yenye kuleta maendeleo na manufaa kwa Tanzania yamefanyika hapa nchini na umeyasimamia na kuyafanikisha ipasavyo” .
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemueleza Balozi Lenhardt leo alipofika Ikulu kuaga na kumshukuru Rais na serikali yake kwa ushirikiano alioupata katika kipindi chake cha ubalozi hapa nchini.
Rais Kikwete amesema ushirikiano wa nchi hizi mbili umekua na kuimarika zaidi na anatarajia kuwa balozi ajaye naye atakuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza na kuimarisha zaidi mahusiano baina ya nchi hizi. Naye balozi Lenhart amesema Tanzania iko moyoni mwake na ataendelea kuwa balozi wa Tanzania popote alipo .
“ Nikushukuru wewe mheshimiwa Rais na serikali yako kwa ushirikiano mzuri na utayari wa kunisikiliza na kunisaidia wakati wote nilipohitaji ushauri wako, umekuwa msaada mkubwa kwangu. Asante kwa ushirikiano wako na siku zote nitaendelea kuwa balozi wa Tanzania kwani Tanzania iko moyoni mwangu”.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu,
Dar es Salaam.
07 October, 2013
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...