BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA)  mapema wiki iliyopita lilikabidhi kibali kwa ajili ya uendeshaji wa Tamasha la Krismasi litakaloendeshwa na kampuni ya Msama Promotions. Tamasha hilo ni muendelezo wa tamasha la Pasaka lililoasisiwa tangu mwaka 2000 likiwa na lengo la kumtukuza na kumtumikia Mungu kupitia nyimbo mbalimbali za waimbaji wa Tanzania na nje ya nchi.


Kabla ya tamasha la Krisimass, Msama alipewa mawazo mengi kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari wa kutoka  vyombo mbalimbali vya habari. Sababu  za kumtaka  Msama  kuandaa Tamasha la Krisimass ni  kupanua wigo wa kuhubiri Neno la Mungu na kuwapa waamini na wadau wa muziki wa Injili fursa ya kupata burudani kupitia nyimbo za watumishi mbalimbali.   



Kampuni ya Msama inayoandaa matamasha hayo mawili yenye mlengo unaofanana, imedhamiria  kuandaa matamasha hayo mawili ni kufikisha neno la mungu kupitia nyimbo sambamba na mapato yatakayopatikana yatasaidia yatima, walemavu, wajane, waathirika wa Ukimwi na wanaoishi katika mazingira hatarishi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hakuna kitu kama Xmass ila Xmas ambayo ni Noeli.

    ReplyDelete
  2. Naipongeza serikali kupitia BASATA kwa kutoa kibali kwa Msama Promotions kuandaa matamasha ya Injili aina hii Pasaka na sasa Christmas.

    Jitihada nyingi zinafanyika kuileta jamii yetu (hasa vijana) katika uadilifu kutokana na mmomonyoko wa maadili. Na ninadhani hayo matamasha ya Injili yanaweza pia kutumiwa kwa lengo hilo. Ikiwa vijana watahubiriwa kwa njia ya uimbaji uzuri wa MUNGU; wakafika mahali wakampenda MUNGU kwa dhati utakujaona hata baadhi ya maovu itakuwa rahisi kuyashughulikia.

    Tabia mbovu haziondoshwi kwa kujenga magereza au kutunga sheria kali, la hasha bali huondoshwa ikiwa jamii itamgeukia MUNGU. Lakini watu hawawezi kumgeukia MUNGU kama hawajasikia akihubiriwa. Na kwahiyo hii nafasi ya matamasha ni "platform" nzuri sana kufikisha ujumbe wa kuasa jamii yetu ili imgeukie MUNGU.

    Napia nimpongeze Msama Promotions kwa jitihada hizo na MUNGU ayafanikishe maono hayo; Jambo la muhimu ni kujitahidi kufanya matamasha hayo kama huduma kwa utukufu wa MUNGU ili kuyafikia makundi yaliyolengwa ili na wao wauone Upendo wa MUNGU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...