Inline image 1
BBQ funga Mwaka iliyofanyika Reading siku ya Jumamosi tarehe 05/10/13 imeelezwa kuwa ni ya mafanikio makubwa. WaTanzania wenye mapenzi na nchi yao walijitokeza na kushiriki kwa pamoja bila kujali dini, itikadi za kisiasa, rangi wala kabila. Waliohudhuria wengi walieleza kufurahishwa sana  kwa mpangilio mzima na kwa wakati mzuri walioupata kubadilishana mawazo na kutafakari mustakabali wa nchi kwa pamoja kama waTanzania.
Inline image 2
Aliyekuwa mgeni rasmi wa shughuli hiyo, Mr Amani Golugwa alitia chumvi na chachu kubwa kwa waTanzania kwa hotuba yake iliyokuwa na weledi wa hali ya juu. Aliwaeleza waTanzania kujihusisha kwa karibu na kushirikiana na wenzao walioko Tanzania katika kutatua changamoto zinazoikabili nchi yetu.  Aliwataka waTanzania hasa vijana kujihusisha kwa namna moja au nyingine katika kuleta mabadiliko bila kujali chama wanachokiunga mkono. Hata hivyo aliwashauri vijana kwamba kama wanaamini katika mabadiliko, itakuwa ni vigumu kuyapata kwa kupitia chama tawala (ccm). Sababu kubwa ni kutokana na kwamba ccm ni chama ambacho kimejisahau na kukua kupita kiasi (too big to change). Kuleta mabadiliko (radical changes) ndani ya ccm ni vigumu sana kama siyo kutokuwezekana.
Inline image 3
Katika siku hiyo CHADEMA imefanikiwa kupata ahadi za mchango wa pikipiki 10 zitakazoelekeza nguvu kwenye kukijenga chama kwenye ngazi za chini (mashina). Pamoja na pikipiki waTanzania wengine waliojitokeza waliahidi kuchangia gharama za ofisi na pango kwenye baadhi ya mashina ya CHADEMA vijijini na mijini pia. Ili kuimarisha na kuiweka CHADEMA tayari kwa ajili ya karne ya 21, baadhi ya waTanzania waliahidi kuitengenezea CHADEMA website ya kisasa kabisa.
Katika kuwavutia waTanzania wasomi na wajuzi ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara, mkutano huo ulidhamiria kuunda chombo cha kisasa kitakachowawezesha waTanzania kuchangia maendeleo ya nchi yetu. Chombo hicho kitakachojulikana kama Center for Leadership and Development (CELEDE), kitawakutanisha waTanzania wote kulingana na fani zao mbali mbali. Taarifa kamili kuhusu hili itatolewa hapo baadaye.
Haya ni baadhi tu ya mambo machache ambayo yanategemewa kufanyiwa kazi siku kadhaa zijazo. Hata hivyo ilikuwa siku nzuri pia kuwakaribisha wanachama wapya (wanawake kwa waume) walioamua kujiunga na chama siku hiyo. CHADEMA ni chama kinachopigania haki ya mTanzania wa kawaida. Namba kubwa ya waTanzania wameshalielewa hilo. Hata hivyo kwa wale ambao bado wanaendelea kudanganyika na hila za viongozi walioko madarakani kwa faida yao wenyewe huku wengi wakiishi maisha duni usiku na mchana, kinachohitajika ni kuwaelimisha. Mwisho wataelewa. CHADEMA kimejitolea na kina nia ya kuendelea kuifanya kazi hii bila kuchoka.
Inline image 4
Aidha CHADEMA UK, wandaaji wa shughuli hiyo wanapenda kuwashukuru sana waTanzania wote kwa kujitokeza kwa wingi kukamilisha shughuli hiyo. Kwa wale ambao wameomba tuandae nyingine kabla ya mwisho wa Mwaka huu, tunawaahidi kwamba mtapata taarifa siku siyo nyingi sana. Itakayofuata itakuwa ni moto zaidi ya hii. 
Inline image 5
Ilikuwa pia ni furaha ni furaha kuwaandaa BAWACHA na BAVICHA ya kesho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. PICHA ZI WAPI ? HAZIONEKANI ? TWAONA KIZA TUU.

    ReplyDelete
  2. Msitari wa chini wa maneno BAWACHA na BAVICHA,,,au BA-BUCHA?

    Sielewi wajameni nimesoma Kiswahili vizuri Shuleni pia nili faulu vema lakini leo kina nigonga, naona shughuli ni ya ulaji wa nyama lakini naona maneno a Siasa au wana maana BA-BUCHA?

    ReplyDelete
  3. Na iwe hivyo BABUCHA lakini shughuli imefana sana mpaka watoto wa Taifa la kesho walikuwa hawataki kuondoka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...