Na Edwin Moshi, Makete
Baada ya zoezi la bomoa bomoa kwa hiari ndani ya mwezi mmoja kumalizika eneo la Makete mjini wilayani Makete, hii leo zoezi hilo limetekelezwa kwa nguvu ya serikali kwa wale ambao hawakubomoa ama kumalizia kubomoa nyumba zao kupisha ujenzi wa barabara ya lami
Ikumbukwe kuwa zoezi la kubomoa kwa hiari lilimalizika Oktoba 09 mwaka huu, ambapo kwa kiasi kikubwa mtandao huu ulishuhudia wananchi wakibomoa nyumba zao wenyewe huku wengine wakitekeleza nusu
Mtandao huu umeshuhudia katapila likiendelea na shughuli ya kupakia masalia ya majengo yaliyobomolewa, huku likibomoa baadhi ya majengo ambayo yalikuwa hayajabomolewa pamoja na yale yaliyobomolewa nusu
Baadhi ya watu walionekana wakiendelea na kubomoa nyumba zao huku wengine wakiokoa baadhi ya vitu ambavyo walidhani vingewafaa kwa shughuli za ujenzi kwenye maeneo mengine
Hii inaashiria ujenzi huo wa barabara kwa kiwango cha lami eneo la Makete mjini unaanza kwa kasi kama inavyotarajiwa na wengi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...