Mkurugenzi wa Kampuni ya Bravo Job Centre, Jaffar Kingwande (kulia), akimkabidhi tiketi Amisa Ally (22), ya kwenda Dubai kufanya kazi ya ndani aliyotafutiwa na kampuni hiyo. Anayeshudia hafla hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana, ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Mohamed Omar. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Jazira Rashid akipatiwa tiketi ya ndege na nyaraka zingine kwa ajili ya safari ya kwenda Dubai kufanya kazi aliyotafutiwa na kampuni hiyo.

 Amisa na Jazira wakiwa na baadhi ya maofisa wa Bravo pamoja na wadhamini wao
Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Omar akifafanua jambo wakati wa kuwaaga wafanyakazi hao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Mungu ni mkubwa sana ila nawaombea hawa DADA zetu wasijekufikwa na mateso kama yanaowafika wengine huko DUBAI

    Jamani tukubali ukweli kuwa hawa waarab kule katika nchi zao wanawanyanyasa sana watu kwa umaskini wao na wanawadhalilisha inafikia wakati unataka kurudi kwenu wanakukatalia na kwa vile wao ndio wana HOLD pass yako ya kusafiria tuwe makini sana na hao watu bora tubakie kwetu tanzania kufanya kazi za ndani kulikoni kwa hao waarabu jamani

    na nyinyi munaojifanya kuwatafutia kazi hao madada zetu huko kama mnaujanja wakuwatafutia kazi watu basi watafutieni nchi za kizungu ambazo zina ubinaadamu kidogo na hata ukitaka kurudi kwenu inakuwa rahisi ukikimbilia kituo cha polisi tu utarudishwa kwenu ila hao waarabu ni WASHENZI sana yaani chozi linanitoka kwani najua hawa madada zetu wanakwenda kuteseka tu na inanisikitisha sana kuwa watu na akili zao wanajifanya ati kuwasaidia watu kupata kazi DUBAI na wananufaika wao kupata pesa wakijuwa fika kuwa huko wanakokwenda hawa madada ni matatizo matupu na wanakwenda kula shida tu mungu mkubwa sana ila sio vizuri kula jasho la mwenzako ambae unautumia umaskini wake kunufaika wewe ....kumbuka kuwa hapa ni mapito tu

    na usitumie umasikini wake alionao kujinufaisha wewe

    ReplyDelete
  2. Hao wanowatafutia kazi ni mawakala ,hivyo wanafanya kwa kulipwa pesa,hawana uchungu na nini kinatokea huko Dubai, wao pesa kwa mbele tu.
    Ni aibu serikali inakubaliana na hili suala mpaka linawekwa bayana wazi kweupe na hakuna wa kutueleza kuwa hao wafanyakazi wa ndani wanafanyaje kama kutatokea matatizo kati yao na muajiri wao.
    Ila kazi ni kazi tu hoja mkono uwende tumboni.

    ReplyDelete
  3. sii mnawahabudi sana niwakatili sana pamoja na dini kuanzia kwao. na mbona hii nafasi naona ni watu wa dini moja tuu kulikoni au ndo kubebana kumeanza.o

    ReplyDelete
  4. Well said mdau watu hawajui maisha ya hizo nchi za waarabu laiti wangejua wazazi wasingekubali kuwapeleka hao mabinti huko.ningekuwa na uwezo wakenya walitengeneza documentary kuhusu mateso wanayowapata,wadada wanaofanyakazi za ndani I wish ingeonyeshwa kwenye televion za Tanzania watu wajionee wenyewe mateso waliyoyapata hao wadada

    ReplyDelete
  5. Nakuunga mkono kwa comments zako. kufanya kazi za ndani kwa namna nyingine ni kama utumwa. mimi lishaishi huko Dubai pia kama myanyakazi wa ndani, kwa kweli yalikuwa mateso matupu hat zangu walichukua mpaka siku ya kuondoka kurudi bongo, mbaya zaidi unaishi na watu usiowajua tabia zao! hivyo watakutumia kadri wanavyoweza wakijua huna kwa kwenda. Najua maisha ni magumu dada zangu lakini lakini hiyo si kazi ni utumwa utaona utakachopata hakilingani na kazi unazofanya na hao wanaowatafutia kazi wananufaika kwa migongo yenu . Anyway good luck!

    ReplyDelete
  6. Ama kweli tatizo la ajira ni kubwa sana hapa TZ.Siamini hata kidogo kama hiyo kampuni haifaidiki na hiyo ajira waliyowatafutia hao akina dada.

    ReplyDelete
  7. anon wa mwanzo,

    kwani kazi za ndani bongo wanalipa laki ngapi kwa mwezi?

    mbona umasikini unatunyanyasa saana kuzidi hata utumwa na ukoloni?

    bora mtumwa aliyshiba kuliko mfanjaa aliye huru.

    ReplyDelete
  8. anon wa mwanzo,

    soko la ajira liko huru. wasipoenda hao wataenda wahindi, wakenya, waithiopia na sisi tutabaki na sifuri maana hamna ajira za ndani hapa nyumbani.

    ReplyDelete
  9. ushauri mzuri ni
    "washaurini watu wakazanie masomo wakiwa shuleni kwani maisha huwa hayana adabu"

    ReplyDelete
  10. wahindi walishapiga kelele saana juu ya mishahara na hali za kazi na walishindwa kwa sababu kuna wahindi wengi mno maskini ile mbaya, huenda wenyewe. kwani hela waipatayo huko kwa hao WASHENZI ni kubwa kuliko waipatayo nyumbani.

    ukitaka uofisa basi soma.

    ReplyDelete
  11. UKWELI:
    1. WATU WAENDA KWA SHIDA ZAO.
    2. ARABUNI NI FURSA AMBAYO TANZANIA NA NCHI NYINGINE MASIKINI HAWAWEZI KUWAPA RAIA WAO.

    ReplyDelete
  12. kwakweli mdau hapo juu amemaliza mengi yale nilitaka andika, Wakenya na waafrika wengine wameteswa,kubakwa, kunajisiwa na hakuna aliye wapa msaada wowote, naomba wale wadau wanaojihusisha na haki za binaadamu walione hili na iwapo hawa ndugu zetu wanaopelekwa huko watanyanyaswa basi hii agency ifunguliwe mashtaka hapo nyumbani.Human trafficking comes in different form, let stop this

    ReplyDelete
  13. Naomba serikali iingolie kati haraka swala hili,tuna mifano hai ya ndugu na jamaa zetu walioteseka kutokana na huo UTUMWA MAMBOLEO.
    Nashanga hata wabunge nao wameingia kwenye biashara hiyo ya HUMAN TRAFFICKING!...Aibu mtu kama ABBAS MTEMVU kujiingiza kwenye Biashara kama hii ya aibu ya UYAYA!....Shame!

    ReplyDelete
  14. Naomba kiundwe chombo cha kuweza kuwa-monitor kikaribu hao Wadada waliopelekwa huko kufanya hizo kazi za kitumwa,ili pindi litakalo tokea la kutokea basi waweze kusaidiwa kurejeshwa nyumbani.
    Nyie mnaojifafanya waratibu hata haya hamuoni kiasi mnajitoa na nyuso zenu kwenye blogs! watu wabaya sana nyie!!! %*@**0)"'"@ zenu

    ReplyDelete
  15. WHAT???????????????? DUBAI?

    ReplyDelete
  16. Hivi kuna shida gani Tanzania hadi wananchi wake wawe exported nje kufanya kazi za ndani!!! huku ni kudhalilisha taifa, mbona kazi za ujasiriamali ziko nyingi? watafute mbinu za kuwafunza ujasiriamali nchi yetu imebalikiwa kuwa na rasilimali nyingi. Wataenda kudhalilishwa kijinsia na waarabu, huo ndio utamaduni wao wa siku zote.

    ReplyDelete
  17. Mwarabu siku zote hajaacha tabia yake ya usulutani! mtu mweusi kwa mwarabu siku zote ni punda tu! poleni sana dada zangu

    ReplyDelete
  18. Jaffar,Amina Ally,Jazira Rashid,Amisa,Sakina, LOL!!!!!

    ReplyDelete
  19. Harafu Mbona hizo kazi ni kwa wanawakeke tu kama hamuendi kuwa ma house keeper sijui au wanaambiwa ni kazi gani?mmh mi inanitia shaka.sijui ngoja tuone

    ReplyDelete
  20. HII INATOFAUTI GANI NA BIASHARA YA UTUMWA!!!!IKOMESHWE MARA MOJA NA SERIKALI IFUATILIE NI WAPI/NINI WANAFANYA HAO MABINTI HUKO.MAMBO YA NNJE MPO????

    ReplyDelete
  21. Yaani hii kampuni inaona ni achievement kuweka taarifa za kuwatafutia kazi za ndani watu.Shameful.
    Hivi wanajua kazi ambazo wanafanyizwa na hawa watu ... it is even shameful to list them here.

    Undertandably, watu watakuwa wanafanya hizi kazi tu kwa kupenda kwao.... lakini si kuweka kwenye mtandao watu wanapewa tickets kwenda kudeki, na kuvua chupi za waarabu huku ndani. Its pity to write but that is what they do over there.

    Ningesikia wamewatafutia hawa dada zetu kazi yoyote bongo i woould not mind. Michuzi do not entartain these type of posting anymore

    ReplyDelete
  22. Utumwa haujaishaga tu? Halafu huu ni wa kujipeleka. Waarabu waonage hivi hivi. Aibu yetu (shame upon us).

    ReplyDelete
  23. NYIE HAMJUI SOKO LA AJIRA ARABUNI.

    MKIZIWIA MASIKINI WENU MJUWE KUNA MASIKINI WENGI DUNIANI WANALILIA NAFASI HIZO.

    ANGALIA MATAIFA YA INDIA, FILIPINO, ITHIOPIA, SUDANI, KENYA, WANAOMBEWA NA SERIKALI ZAO.

    ReplyDelete
  24. kazi ya uyaya bongo hailipi kama dubai.

    mkiwazuia watu wasiende kwa chuki zenu mtawalisha?

    waache wajitegemee.

    ReplyDelete
  25. Hii si kesi ya kwanza, Swala hili linastahili kufikishwa bungeni lijadiliwe, ulizeni wakenya,Philipines. Kama ukiona Documentary utaona uchungu!! jinsi watu wanavyotendewa. Ukweli nchi za kiarabu mtu mweusi ni mtumwa!! na hakuna human rights, TZ haitakuwa na uwezo wa kumsaidia yeyote atayepata matatizo.! Kampuni husika iwe Responsible kwa lolote litalotokea, Ifunguliwe mashtaka!!

    ReplyDelete
  26. mbona kelele nyiingi, wenzenu wamepata ajira au mwawaonea wivu! mnataka wakajipange barabarani kuuza miili yao!!!! hawakujaaliwa elimu ndo maana wametafuta kazi za ndani, hata nyie mmeajiri wadada pia wanawafanyia kazi majumbani,khaa... mnachonga sana

    ReplyDelete
  27. HUU NI UTUMWA WA KISASA AMBAO WAJANJA WANAUTUMIA KUPITIA MGONGO WA CCM KAMA TULIVYOKWISHA SHUHUDIA MHE. MTEMVU MBUNGE WA TEMEKE AKIJIVUNIA KUWAPATIA HIZO KAZI.HAWA HAWANATOFAUTI NA WANAOSAFIRISHA WASICHANA WA KAZI ZA NDANI TOKA MIKOANI, SETRIKALI IINGILIE KATI NA IWAREJESHE WALIOPELEKWA NA MTEMVU.

    ReplyDelete
  28. Hebu jamaani kabla. hamjawasafirisha ndugu zetu huko kwenye nvhi za warabu muwe kwanza mnafanya uchunguzi angalau, maana hata you tube zinaonyesha baadhi ya mataifa ya Africa waliopelekwa huko Kwa kazi kama hizi, tupendane wandugu, mateso ni kitu kibaya, warabu wengi wao kwanza hawamthamini mtu mweusi, wanamuona kama mtumwa, wana unyanysaji na ubaguzi, wako tayari kumthamini mtu mweupe. yaani Mzungu, lakini sio african mweusi, tusipo jipenda yaani kuthaminiana sisi Kwa sisi nani? atatuthamini sisi weusi, hizi kazi ni za kitumwa huko

    ReplyDelete
  29. Kenya mwaka juzi ilisimamisha ruksa ya kupeleka watu katika nchi moja ya uarabuni kwa vile wapo walionyanyaswa hata kupoteza maisha. Wapo walioenda wakapata waajiri wazuri waliofanikiwa kuinua maisha ya jamii zao. Ingawa ni rahisi kuwasema mawakala ukweli ni kwamba usipompatia mtu kazi mbadala unakuwa hujamsaidia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...