![]() |
Bundi mtuhumiwa mwenye jina la UdiUdi anayemilikiwa na Ras Makunja |
Wiki endi haikuwa nzuri katika makao ya mkuu wa FFU Ughaibuni kamanda Ras Makunja, baada ya mmoja ya majirani kulalamika kuwa ndege aina ya Bundi anayefugwa katika kasri la Anunnaki Empire analoishi mwanamuziki kamanda Ras Makunja kiongozi wa Ngoma Africa band kule ujerumani.
Bundi huyo sasa amekuwa na tabia za ukwapuzi, Jumamosi
iliyopita alishutumiwa kuiba viatu na jozi ya soksi za jirani , jirani anadai kuwa Bundi huyo aliruka hadi kwenye bustani ya jiarani na kukuta viatu vya kuchezea mpira vilikuwa vimesauliwa nje na kuruka navyo ! kitu amabcho si cha kawaida.
Jirani alidai ndani ya viatu pia kulikuwa na soksi vyote hivyo vilikutwa juu ya paa la Bundi huyo baada ya Askari wa kikosi maalumu cha kuangalia wanyama kumfatilia Bundi huyo aliyepewa jina la Udi Udi.
Jirani alilalamikia kuwa huyu Bundi siku hizi ni mdokozi na kwa nini asihamishwe arudishwe Zoo??
Cha kushangaza shutuma za jirani zilitupiliwa mbali na maaskari hao na badala yake jirani kapewa Onyo kwa kuambiwa asijaribu kumrushia hata jiwe Bundi huyo.
Askari hao wamesema Bundi wa kamanda anaruhusiwa kuwa huru majira ya jioni kwa ajili ya kuruka kupunguza uzito na kupata
hewa mwanana.
Jirani huyo alibaki mdomo wazi na kushikwa na mshangao kwa kuambiwa kuwa Bundi hakuiba viatu Bali aliokota,na akamua kuvipeleka juu ya banda lake, kwa kuwa mmiliki wa Bundi huyo ni
jirani mwema lazima viatu angevurudisha kwa mwenyewe au kuvipeleka ofisi maalumu ya vitu vya kuokota (Fondbureu).
Jirani haelewi pale wanausalama hao wa wanyama walipomwambia ole wake kama Bundi huyo akikutwa na jeraha.
Mmliki wa dege hilo la kutisha baba mtukutu kamanda mkuu Ras Makunja wa FFU, hakuwa a mengi ya kusema Bali alimuomba ladhi jirani huyo kwa kumwambia ondoa shaka huyu Bundi sio mkorofi bali ni rafiki wa Kila mmoja. Pia jirani aliambiwa na kamanda kuwa na yeye ajaribu
kuomba kibali cha kufuga mwewe au kunguru kwani ni ndege wazuri tu kamanda aliongeza ndogo kwa jirani huyo.
Kamanda Ras Makunja akiwa mbele ya makazi ya bundi wake udi udi
Ninaomba Uwakili wa kumtetea Bundi wa Ras Makunjas.
ReplyDeleteNitasafiri kutokea Tanzania hadi Berlin Ujerumani na kusimama Mahakama ya wanyama kumtetea Bundi wa Mamlaka ya Anunaki ya kuwa hakupewa malezi mabovu na Ras Makunjas kiasi cha kufanya kosa hilo !
Hao askari wa wanyama pori hawakukamilisha kazi. Walitakiwa wafanye utafiti ni nini kilimvutia bindi kuiba viatu. Wangevinusa hivyo viatu tu wangejua sababu. Bundi ni jamii ya ndege wala nyama, alijua kashaokota mzoga!!!
ReplyDeleteMdau wa pili hapo juu, ina maana viatu vilikuwa vinatoa harufu ya mzoga? Ndio maana akavutiwa na hiyo harufu au?
ReplyDeletesio bure bundi alitumwa na maafande wenyewe wa ffu,mbona tumesikia udaku kuwa bundi wenyewe amekuwa akianua anua nguo za majirani pia
ReplyDeleteImani ya kijadi ya kwetu (pamoja na huyo Ras...)ni kuwa bundi akikufanzia jambo...LO! NI UCHURO HATARI SANA!!Mbona amemletea mtoto wa watu majanga. Mwanzo viatu,soxi,itafuata...LO!....(subirini).Ni bora ampeleke ZOO huyo ndege mapema..:maana hana uwezo wa kumfuga.
ReplyDeletelakini cha kushangaza yule bundi ndani ya "Anunaki Empire" nafanya kazi gani? au ni halama ya nini?maswali mengi najiulizalakini sipati jibu,na kuwavaa Ngoma Africa bendi au FFU kuwauliza kulikoni kwa Boss yao kuwe na bundi naogopa kisago,jibu sipati.
ReplyDeleteMdau wa BREMEN
Naona jirani kaingia katika himaya
ReplyDeleteya mtandao wa viumbe wa ajabu FFU,chini baba mtukutu kamanda ras makunja mmiliki wa Anunnaki Empire.
Kitakachofuatia inawezekana jirani akambiwa ahame na askari,kama anaona bundi ni kero,wazungu viumbe wa kushangaza sana wanathamini mdudu kuliko mtu.
ReplyDeleteyule bundi inasemekana alikulia pale tangu akiwa mdogo na kazoeana sana na majirani,sema tiu hizi tabia za udokozi kanzia ukubwani
ReplyDeleteBundi ndani ya 'Ananuki Empire' ni alama kubwa sana hata kwa Wajerumani wenyewe ni vile yupo kwenye ADAMU NA HAWA YAO kama ile ya kwetu JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
ReplyDeleteAngalia Nembo ya Ujerumani utaona alama ya NDEGE!
Bundi wa Ananuki Empire ni TAMBIKO LA KIAFRIKA !
ReplyDelete