CHADEMA UK inawakaribisha waTanzania na wapenzi wote wa CHADEMA kwenye barbeque (End of the Year BBQ) party itakayofanyika Comunity Hall/Back Garden, 44 Watlington street, RG1 4RJ Reading tarehe 05-10-2013.

Mgeni rasmi atakuwa ni mwanasiasa mwenye kipaji cha pekee na muhimili muhimu wa CHADEMA – katibu wa CHADEMA Arusha na kanda ya kaskazini ndugu Amani Golugwa.

Itakuwa ni siku nzuri kujiburudisha kwa nyama choma, vinywaji na muziki free of charge. Lengo ni kuwakutanisha wapenda maendeleo katika kubadilishana mawazo na kujumuika katika harakati za kimaendeleo kwa taifa.

Hii shughuli si kwa wanaCHADEMA peke yake. Kila mTanzania mpenda maendeleo anakaribishwa kuhudhuria. Ni wakati mzuri kukaa pamoja tukijiburudisha huku tukibadilishana mawazo on party lines kiutu uzima bila malumbano. Wakati ni huu kuonesha utashi na ukomavu wa kisiasa.

Chakula na vinywaji bure!!!

Karibuni wote

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mtaishia kufanya Matamasha ya Nyama Choma, ndio Harakati zilizobaki kwqenu baada ya kufilisika Kisiasa.

    Mkiingia Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 mtapata Namba za Viatu !!!

    Kama Chama cha Siasa kitatoa Huduma ya BBQ (Nyama Choma) je Hoteli, Migahawa na Misururtu ya Mama Lishe wao wakale wapi?, mtawapa kazi gani mbadala?)

    Sasa Uchomaji wa Nyama na Siasa wapi na wapi?

    ReplyDelete
  2. Ai nyawe, ng'waitu iha-Golugwa. Umunyihansu ne gwa? Angazetai, hamila ku namba ing'wi jamani, mbona nziza iite uuuh" Une kituitu ku-Ibaga, Mkalama, lakini aintugilwe Kihanzu na jamii kubwa iko huko. Haya ikiie uza gwa! Bye dear.

    ReplyDelete
  3. Haiezekani Chakula na Vinwaji kuwa bure, je awi la Chama UK litakusanya vipi fedha za kujiendeshea?

    Au ndio vile kama mnavyodaiwa CDM mnadhaminiwa na NGO's na Makanisa ya Ulaya?

    ReplyDelete
  4. Mtachoma saaana Mishikaki na Nyama Choma na ktk Siasa na Uchaguzi mataishia kuburuzwa na CCM !!!

    ReplyDelete
  5. Mbona mapema hivyo? Mwisho wa mwaka???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...