1) Mume Kuoa Mke Mwengine Bila Ya Yule Wa Kwanza Kujua
Swali:
Inajuzu kwa mwanaume kuoa mwanamke mwengine bila ya kujua yule mke wa kwanza? Ni kwa kuwa alimuahidi yule mke wa kwanza kwamba hatooa mwengine.

´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Ikiwa alimuahidi, basi ni wajibu kutimiza ahadi.
"Enyi mlioamini! Timizeni mikataba." (05:01)

Ikiwa alimpa ahadi, basi anawajibika asioe mwengine.

Muulizaji:
Na ikiwa hakumuahidi?

´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Ikiwa hakumuahidi, anaweza kuoa.

2) Kuoa Mke Wa Pili Bila Ya Mke Wa Kwanza Kujua

Swali:
Je inajuzu kwangu kuoa mke wa pili bila ya mke wa kwanza kujua kwa kuwa wa kwanza haridhii?

´Allaamah Swaalih as-Suhaymiy:
Kwa nini unasikia uoga? Kwa nini? Wengi wetu ni waoga katika masuala haya. [Wanasema] "Msiwaambie wanawake kwa kuwa hawatokubali hata Hadiyth."

Ndugu wapenzi! Mke wa kwanza hana haki kukukataza au kukuingilia baina yako wewe na baina ya kuoa, lakini wewe sasa iulize nafsi yako. Ukikuta kwenye nafsi yako wewe ni mwanaume mwenye uwezo wa [kutekeleza] uadilifu na moyo wako ni wenye nguvu, na utaweza kuvumilia utayosikia na kukabiliana na maneno mengi, jitahidi kwanza kwa uadilifu, kisha ndio uoe zaidi. Ama ikikujia katika nafsi yako dhana kuwa utalemea moja kwa moja kwa [mke] mmoja na unakhofia matokeo mabaya, usifanye hivyo.
Mimi nafikiria ikifikia suala la wewe mpaka kukhofia utapomueleza hali itakuwa khatari sana - ni juu yako kuwa mpole kwake, panga utayomwambia, jitahidi kumuweka katika hali nzuri, mfurahishe kwa kitu chochote kama mali n.k. Kisha ukihakikisha ukaona kuwa hajaridhia, yaani haikuwezekana kukubaliana na wewe juu ya hilo, sio lazima kwake kukukubalia.
Na [wanaume] huisheni hii Sunnah! Wanawake wa Kiislamu wamekaa manyumbani, [mpaka] miaka ya kuolewa inapita. Baadhi ya manyumba yana wanawake kumi, miongoni mwao kuko wanaofika hadi miaka arubaini mpaka khamsini na wala hawajaolewa. Na sisi tumewaiga wamagharibi na tumekaa kazi tu ni kusikiliza filamu chafu - na mafilamu yote ni machafu ambayo yanashawishi suala la ndoa, ukewenza n.k. Na Allaah (´Azza wa Jalla) Anasema
"... Basi oeni mnaowapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane." (04:3)
Kaanza kwa wake wawili. Na nnakumbuka kuwa Shaykh wetu Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) na hata Salaf katika hili wanasema:

"Asili ni [kwa mwanaume kufanya] ukewenza."
Kuondolewa ukewenza ni wakati wa khofu tu, khofu ya nini? Kutekeleza uadilifu tu.

Chanzo:
http://youtu.be/WRcQZr1IQYk

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Swadaqta!

    TUKUMBUKE MTU UNAWEZA KUAHIDI LAKINI UKAONA MATUNDA YALIYO PENDEZA UKAZIDIWA NA UKAKIUKA AHADI:

    Je, hata kama uliahidi kotooa na ukakiuka ahadi Ukaoa je una adhabu gani?

    ReplyDelete
  2. SAMAHANI JAMANI MIMI MKIRISTO HIVI NAWEZA BADILI DINI ILI NIOE MAANA DHAMBI HII TU NDIO NAHISI INANIKOSESHA AMANI NA MUNGU DAH JAPO WAWILI BANAH HUYU MMOJA HATOSHI, NAOMBENI USHAURI

    ReplyDelete
  3. Na Ndiyo maana siku hizi utasikia wanawake ambao wameolewa na waume wawili.......mmezidi kutuonea! Wanaume wengine hata uwezo wa kutunza wanawake wawili au kuwaridhisha kimwili hawana, lakini utakuta wanaoa bila sababu za msingi kama zilivyoandikwa kwenye vitabu. Hakuna mwanamke duniani anayetaka au kupenda uke-wenza, awe mwislamu asiwe mwislamu. Ni kusononeshana tu na mungu hapendi.

    ReplyDelete
  4. Kwakweli wanaume wengi wanaegemea katika suala la kuruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja lakini hawatazami yanayoambatana na sunna hiyo. Kwa mfano mwanamme haswali, funga yake mtihani, utekelezaji wa majukumu yake kwa huyu alienae ni mtihani lakini utakuta huyu huyu anasema anataka kuongeza mke wa pili????? Hebu kuweni waadilifu na wale mlionao ki Lillah muone kama mtatamani kuoa mke mwingine!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...