MBU ni tatizo kubwa kwa afya zetu na familia zetu kwa ujumla.Tokomeza maleria kwa kutumia dawa ya asili iliyotengenezwa kwa mitishamba Dawa hii ukishaiweka kwenye umeme inatoa harufu nzuri isiyokuwa na kero, ambapo husababisha mbu kuikimbia harufu hiyo.
Unaweza kuacha mlango wazi na mbu hukimbia kwenda nje, na walio nje hawewezi kuingia ndani kutokana na perfume inayotoka kwenye dawa hii. Kumbuka kuwa mbu huingia ndani kwa wingi mida ya jioni giza linapoanza na asubuhi kunapoanza kupambazuka, muda huo kama utakuwa umewasha dawa, hata ukifungua milango mbu hawataingia ndani. Haina madhara kwa afya ya mwanadamu kwa kuwa imetengenewa kwa miti shamba na products nyingine za asili.
Machine pamoja na dawa Tsh 25,000/=. Dawa (liquid) peke yake Tsh 10,000
Sabuni bei yake ni 5000/=.sabuni hii haina madhara hata kwa mtoto mchanga imetengenezwa kwa miti shamba. Hii ni Sabuni nzuri sana kwa ajili ya kufukuza mbu, ukiitumia kwa kuoga inaacha harufu mwilini ambayo mbu huikimbia harufu hiyo. Sabuni hii pia ni nzuri kwa ngozi, pimples na mabaka/madoa kwenye ngozi huondoka. Haina madhara kwa afya ya mwanadamu kwa kuwa imetengenewa kwa miti shamba na products nyingine za asili. Mtoto mdogo anaweza kuitumia sabuni hii. Familia yangu tunatumia sabuni hii.
Kwa anayetaka kuwa supplier au kununua
Tuambie kuhusu kuthibitishwa na TBS
ReplyDeleteWatu wengu wana aleji ya pafume. Je hii haitawadhuru?
ReplyDeleteJe ina viwango vilivyopimwa?
Mti upi? Na pia TFDA wameithibitisha mana isije ikawa kama ya mafuta ya ubuyu, yale yale! watu watumie mwisho wa siku oh haifai kwa matumizi ya binadamu. Mana huo moshi wake ndio mpango mzima katika kuvuta, je mwilini hakuna tatizo, mdau juu
ReplyDeletealivyosema allergies nk?
Je, imethibitishwa na TBS? Maana kutengeneza na miti shamba si hoja. Kwa kuwa dawa nyingi zinatokana na miti shamba, isipokuwa zinawekwa ktk maumbo fulani fulani kwa kutumia mashine.
ReplyDeleteMimi utaweza kunishawishi utakapoonesha alama ya TBS
Nyinyi mmesoma Maelezo!! Mshaambiwa haina MADHARAAA!!!
ReplyDeleteSio mtu atuambie haina madhara maana kila mfanya biashara atasema hivyo, tunataka tuambiwe na trusted source kama TBS, TFDA n.k. Apeleke hiyo perfume na sabuni vikafanyiwe utafiti.......
ReplyDeleteni kweli kabisa kupata uthibitisho kutoka taasisi za Serikali sio kwa mfanyabiashara kwa maneno ya kibiashara.
ReplyDeleteHebu wa-scan vyeti vya TFDA na TBS tupate uhakika.
ReplyDelete