Mkuu wa wilaya ya Ruangwa akizungumza na Watumishi wa  Kata 9 Katika Tarafa ya Ruangwa ikiwa ni mkutano wake wa mwisho kukutana watumishi wa Umma katika wilaya hiyo,Wengine kutoka kushoto ni kaimu Afisa elimu na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bw Reubern
Mfune
 Mkurugenzi mtendaji wa Ruangwa,Reabern Mfune akieleza mipango ya
halmashauri hiyo kwa kila kata kwa mwaka huu wa Fedha
  wadau-Baadhi ya watumishi wa halmashauri ya wilaya kutoka kata 9
za Taraf ya Ruangwa walipokuta na mkuu wa wilaya.
=======  =======  ======
Wakuu wa Idara na Vitengo katika Halmashauri ya Wilaya  ya Ruangwa
Mkoa wa Lindi wametakiwa kuacha vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa
na baadhi ya wakuu hao kwa watumishi wengine wa Kada za Chini na
kusababisha kuzorota kwa utendaji wa kazi hali inayosababisha jamii
kutopata huduma ipasavyo na kuichukia Seikali yao

Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Ruangwa,  Agnes Hokororo katika
kikao cha mwisho  kilichofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa
halmashauri baada ya kukamilisha kukutana na watumishi mbalimbali wa
Umma wa halmashauri hiyo

Baadhi ya watumishi hasa wa idara ya elimu walilalamikia vitendo
vinavyofanywa na wakuu wa vitengo na wa idara kuwanyanyasa kwa lugha
chafu hata mbele ya wanafunzi  hali hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa
kuzorotesha maendeleo Hususan katika Kada ya ualimu.

Hokororo alisema kuwa jukumu la viongozi ni kuwa karibu na wale
waliochini yao na kuonesha ushirikiano  na ili kuleta ufanisi katika
eneo la kazi na si kuonesha vitendo vya unyanyasaji.

Alimtaka Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,Reuben  Mfune
kufuatilia tuhuma hizo na kuwachukulia hatua wale wota watakaobainika
kuwa na tabia za kuwanyanyasa walio chini yao ‘Ded hakika tulikuwa wote kwenye mikutano hii na umesikia mwenyewe watumishi walivyokuwa wanasema Fanyia kazi na ndio lengo la kufikia na kupata matokeo bora sasa Imenisikitisha sana kusikia unyanyasi wa wakubwa wa Idara …Alimalizia Hokororo.

 Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Reuben Mfune aliahidi
kufanyia kazi malalamiko hayo ya watumishi hao  na kuwataka watumishi
hao kuendelea na majukumu yao kwa lengo la kufikia ufanisi.

Aidha Mfune alieleza kuwa Halmashauri yake imejipanga kutatua kero za
watumishi ikiwemo vitendea kazi,malazi na Malipo ya usumbufu na Likizo
na kuhimiza watumishi hao kutekeleza wajibu wao ili kuimarisha Wilaya
hiyo inayokuwa kiuchumi

Katika ziara hizo Mkuu wa wilaya aliweza kukutana na watumishi walio
katika kata zote 21 za Wilaya hiyo hivi karibuni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...