Na Abdulaziz Video, Lindi
Mtu mmoja aliejulikana kwa jina la Burhan Islam ambaye ni fundi wa magari, amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria aina ya Fuso
kugonga lori lingine nae kubanwa na bodi na kuokolewa baada ya
jitihada zilizofanywa na baadhi ya Abiria waliokuwa wakisafiri katika
barabara kuu ya Dar es salamu kwenda Mtwara na Lindi.
Gari hilo lenye namba za usajiri T 56ANQ lililokuwa likiendeshwa na
Kunja Mshamu limepata ajali hiyo leo katika kijiji cha Mkwajuni
wilayani Lindi baada ya kutaka kulipita gari lenye namba za usajili
T 402 AJG Scania lililokuwa likiendeshwa na Amos Chadenyile.
Majeruhi huyo baada ya kuokolewa katika ajali hiyo alikimbizwa katika
kituo cha afya Kitomanga kwa huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa
katika hospital ya Mkoa wa Lindi kwa Uchunguzi zaidi. Katika ajali hiyo iliyousisha malori hayo hakuna mtu mwingine
aliyejeruhiwa huku gari hiyo ya Fuso likiwa limeharibika sana
Wasamaria wakifanya juhudi za kumnasua Burhan Islam
Majeruhi Burhan Islam baada ya kuchomolewa sehemu aliyokuwa amenasa na kabla ya kukimbizwa kituo cha afya kwa huduma ya kwanza


Pole sana Burhan - Mungu ameyanusuru maisha yako!
ReplyDelete