Rais wa Serikali ya Wanafunzi Madaktari wa Chuo cha Bugando (CUHASSO) Musa Leonard Mdede (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa tamko kwa niaba ya wanachuo kuiomba Serikali kutoa udhamini wa ada kwa asilimia 100 kwani wanafunzi wengi wanashindwa kumaliza masomo yao kutokana na kujikita kwenye shughuli za usakaji pesa kwaajili ya malipo, nazo ada zikiendelea kupanda kila misimu huku Serikali ikiendelea kutoa ufadhili kwa asilimia ileile.
|
"Tunaiomba Serikali kuongeza kiwango cha ufadhili ili wanafunzi au vijana walio na nia ya kusoma fani ya udaktari wakiwa wanalenga kuokoa maisha ya watanzania watimize ndoto zao. Tunatambua kuwa nchi yetu ina upungufu wa asilimia 60 ya madaktari wa sekta ya afya"
"Na kwa takwimu daktari mmoja anahudumia zaidi ya wagonjwa 33,000 kutokana na idadi ya watanzania wote, sasa kuendelea kuwa na vijana wanaoshindwa kuendelea na masomo ya sekta ya afya kwa sababu ya kukosa karo, nikurudi nyuma na kamwe malengo hayatotimia" Alisema Musa Leonard Mdede
|
Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi Madaktari wa Chuo cha Bugando (CUHASSO) Atukuzwe Mordekai Gwihangwe (katikati) akitoa ufafanuzi jinsi ada kubwa inayotozwa kwa wanafunzi inavyokwamisha malengo ya wanafunzi wa sekta ya Afya nchini hali inayopelekea serikali kukosa wataalamu wa kutosha. Kushoto ni Rais wa CUHASSO Musa Leonard Mdede na kushoto ni Benjamin Thomas.
|
Ndugu wana habari,napenda kuchukua nafasi hii kama Rais wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu katoliki cha sayansi ya Afya na Tiba(CUHAS-Bugando) kwa niaba ya wanazuoni wote wa chuo hiki na kwa niaba ya wanafunzi wa sekta ya Afya wa vyuo vikuu vyote visivyokua vya umma nchini(yaani vyuo vikuu vikuu vyote vya fani ya afya vinavyomilikiwa na mashirika ya dini na mashirika ya watu binafsi).Kuweza kueleza kilio chetu kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vyombo mbalimbali vya kiserikali vyenye mamlaka ya kusimamia Elimu ya juu na vyuo vikuu nchini.
I:DHANA YA ASILIMIA MIA MOJA YA MKOPO.Watanzania wengi wakiwemo ndugu na jamaa wa karibu wanaotugharamikia katika masomo yetu wanaelewa kwamba mwanafunzi anayesoma fani za Afya kama Udakatari,Ufamasia,Uuguzi na nyinginezo kama hizo analipiwa kila kitu na serikali kupitia bodi ya mikopo kwa hiyo hahitaji msaada wowote wa kifedha kutoka kwa wazazi au walezi kwa kua anjitosheleza kwa kila kitu.Dhana ambayo kwa mwanafunzi anayesoma katika chuo kikuu kisichokua cha Umma ni tofauti kabisa.Kwa kua asilimia mia moja inayoongelewa ni kama asilimia hamsini tu ya karo zinazotozwa katika vyuo hivi.
Wanafunzi wote wa vyuo hivi vya fani ya Afya visivyokua vya umma tumekua tukipokea kiasi cha shilingi za kitanzania milioni mbili na laki sita tu(Tsh.2,600,000/=) toka bodi ya mikopo kama mkopo kwa ajili ya Ada.Kiwango hiki kipo hivo toka wakati huo ambapo katika vyuo hivi Ada ilikua inatozwa kwa kiwango hicho.Ni takribani miaka sita sasa kiwango hiki kimebakia kama kilivo bila kuongezeka.Wakati kutokana na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji wa taasisi hizi.
Ada zimekua zikiongezeka mwaka hadi mwaka na sasa kufikia takribani milioni nne,na zaidi kama karo katika vyuo hivi mbalimbali Ikiwa ina maana kwamba kiasi kinachobaki baada ya Tsh.2,600,000/= kutolewa kama mkopo mwanafunzi mwenyewe inatakiwa ajilipie pamoja na gharama zingine ambazo si sehemu ya karo zinazohitajika kutolewa.Wanafunzi wengi katika vyuo hivi wanasoma na kuishi katika mazingira magumu sana kwa kua gharama anazotakiwa kuchangia binafsi ni kubwa kiasi cha kuwalemea wanafunzi wengi ambao wengi wetu ni watoto wa wakulima ila tukiwa na haki ya kupata Elimu bila kujalisha hali ya uchumi wa familia zetu
.CHANGAMOTO;hali hii imepelekea wanafunzi wengi wanaochaguliwa kushindwa kujiunga na vyuo hivi kwa kushindwa kumudu gharama hizi,lakini pia imepelekea wanafunzi wengi kupoteza mda wao mwingi katika kufanya vibarua ili kupata kiasi cha kumalizia ada ambayo imepelekea ufaulu wao kushuka na wengine kupoteza kabisa nafasi ya kuendelea na masomo.
OMBI LETU KWA SERIKALI;kwa kua tumejiunga na vyuo hivi kwa mfumo halali wa Tume ya vikuu Tanzania(TCU) ambao haukuangalia hali ya kiuchumi ya familia zetu kama tutamudu au hatutamudu kulipa gharama hizi,kwa kua tulijiunga na vyuo hivi kwani tulikua na vigezo vya kusoma fani hizi kama wenzetu wanaosoma katika vyuo vikuu vya umma na hata zaidi na kwa kua tukihitimu sisi wote yaani wenzetu wanaosoma vyuo vikuu vya umma na sisi tunaosoma vyuo vikuu visivyokua vya umma tunakwenda kuhudumia na kuokoa uhai wa watanzania walewale.
Tunaiomba serikali iongeze kiwango hiki tunachopewa kama mkopo kwa ajili ya ada,ili hiyo Asilimia mia moja inayosemwa iwe na maana kwetu kwa kua kwa sasa ni kama nusu tu.Wengi wanashindwa kujiunga na vyuo hivi kwa kushindwa kumudu gharama hizo.Katika nchi yenye upungufu wa 60% ya madaktari na wataalamu afya kwa ujumla,pia katika nchi ambayo daktari mmoja anahudumia wagonjwa zaidi ya 33 elfu.Si vema kuona vijana wenye dhamira na nia thabiti ya kuokoa maisha ya watanzania wanashindwa kutimiza ndoto hizo za kua wataalamu wa Afya ati kwa kushindwa kulipa karo.
Tume ya vyuo vikuu Tanzania(TCU):Upandishwaji Ada katika vyuo vikuu visivyokua vya umma usiofuata utaratibu na Kile kinchojulikana kama “List of Approved programme fees” ikiainisha gharama za ada zinazotozwa katika vyuo vikuu vyote nchini.Tume vya vikuu Tanzania imepewa mamlaka kisheria kwa mujibu wa sheria ya vikuu No.7,2005.Kusimamia kuanzia udahili na uendeshaji wa vyuo vikuu vyote nchini vya umma na visivyokua vya umma.Central Admission system
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII;Institute of Health and Allied Health sciences.
Kumekuwa na changamoto kubwa katika gharama za ada, chakula na makazi kwa wanafunzi wa stashahada katika vyuo vya Afya hasa vile vya binafsi ambapo gharama za uchangiaji zinazidi kuwa kubwa ikizingatiwa kuwa wanafunzi hao hutejigemea kiasi kikubwa na kuwa serikali kupitia wizara ya afya imekua ikitoa fedha kwa ajiri ya wanafunzi hao.
OMBI LETU:-Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kuweka wazi ni kiasi gani inachangia kwa kila mwanafunzi mmojammoja wa stashada katika vyuo vya afya kwa kueleza mchanganuo halisi ili kuwawezesha wanafunzi hao kutambua ni kwa kiasi gani Serikali kupitia wizara ya Afya na ustawi wa jamii inachangia kama ulivyo utaratibu wa bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa shahada .
Vilevile kumekuwa na changamoto ya mabadiliko ya gharama za ada kwa wanafunzi wa stashahada katika vyuo vya afya na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wanafunzi hao hivyo Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Kutoa gharama halisi ambazo wanafunzi wa stashada katika vyuo vya Afya watapaswa kuchangia katika vyuo mbalimbali ikiwemo vile vya binafsi.
Kulingana na changamoto mbalimbali zinazozidi kujitokeza kwa wanafunzi wa stashahada katika vyuo vya afya, Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Kuboresha mfumo wa uwezeshaji kwa wanafunzi wa stashada na kuweka mfumo na taratibu zitakazosimamia mabadiliko ya ada katika vyuo mbalimbali vya Afya ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza vyuoni hasa vya binafsi.
Kumekuwa na uchakavu wa miundombinu inayomilikiwa na wizara ya Afya katika vyuo vya afya na hivyo kupunguza ufanisi wa masomo kwa wanafunzi hivyo Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Kuboresha miundombinu mbalimbali inayomilikiwa na wizara ya afya katika vyuo vya Afya vinavyotoa stashahada.
hii kali ya mwaka, si tuna uhaba wa madaktari sasa ya nini kutowapa asilimia 100 ya mkopo. kwa hiyo ni waalimu tu ndio wanapewa asilimia 100 ya mkopo. jamani tukitoka hapo tunalalamika nje tuna uhaba wa madaktari! hivi hii imekaaje? Serikali iliangalie kama wanafunzi walivyoomba.
ReplyDeleteNinyi vijana acheni kupenda vya bure. Kila kitu serikali, wazazi wenu wako wapi au ndugu na walezi wenu. Nani aliwatuma wawe maskini?
ReplyDeletePesa mkikopeshwa hamrudishi...sasa mnategemea nini, kila siku kulia tu. Barabara zisijengwe, huduma za afya mbovu, kisa ninyi wapenda ngono. Huko chuoni wanaosoma wachache, na hao wachache wamepewa scholarship wapo marekani au uingereza na nchi nyingine. Sasa nyinyi kwa sababu hamkuwahi kuwa shule special, kama mimi za Ilboru, Mzumbe, Kibaha au Tabora, bado mnataka mthaminiwe kama sisi special.
Wakati si tunasoma usiku, nyinyi mlikuwa mnazurura usiku na wanawake. Leo mnataka msome bure.
Mi niko against serikali kuwabeba watoto wa namna hii. Hata mimi wazazi wangu walikuwa maskini, na nililitambua hilo nikaongeza juhudi, mpaka nikaenda special Ilboru na leo nafanya PhD hapa Stanford Uingereza. Mda wote wakati mi nasoma, marafiki zangu walikuwa wanabadilisha msichana huyu na yule. Walivyofeli, wakawa nalalamikia seriikali, eti hakuna shule za kutosha. Sasa kama hakuna shule za kutosha kwa nini wasingejitahidi ili wapate nafasi katika shule hizohizo chache zilizokuwepo? Mbona wengine walipata, pamoja na kwamba hawakuwa special kama mimi.
Anonymous wa pili
ReplyDeleteNina wasiwasi na shule yako kama kweli imekusaidia. Naona wewe ni kati ya wale watanzania waliopata nafasi za kusoma nje ya nchi mpaka PhD lakini wameshindwa kuleta mabadiliko nyumbani.
It's time for a change now. We need to workout on how to reform our policies, to support all Tanzanians get a better education. Hivi unafikiria hao waliofeli, au waliokuwa wanatembea na wanawake was their choice? au unafikiri wewe unayesoma UK ni kwa sababu ya juhudi binafsi tu? Naamini kwa sasa utakuwa unaelewa kitu kinachoitwa "social determinants" au "social ecological model" when it comes to inequity.
Mimi nimesoma Tabora pale, na sasa niko nje nafanya Masters yangu. Lakini nimekuja elewa sina tofauti na yule aliyesoma shule nyingine au anayesoma chuo chochote Tanzania.
Cha zaidi ni kujitahidi jinsi ya kubadilisha mambo pale nyumbani.
Hili swala la fee kwa wanafunzi wa fani za afya ni la kufanyia kazi, ukizingatia vijana wana-apply kupitia TCU, kwa hiyo siyo wenyewe wanaochagua kwenda kwenye vyuo vya umma au binafsi. Otherwise serikali irudishe utaratibu wa zamani vijana waaply directly kwenye vyuo.
Kwa ujumla kuna umuhimu mkubwa serikali kulipia kwa asilimia 100% gharama za fani za afya.
Kazi ipo! Kwanza nawapa pole hawa wasomi na ninawapongeza kwa kupigania haki. Wewe msomi wa PhD Stanford Uingereza pole sana, kwa mtazamo wangu inaonekana bado hujuwa na uwezo wa kupambanua mambo kulingana na jinsi ulivyoongeza elimu ya madarasani. I have doubt over your education if will be productive within our contemporary society. I can advice you on top of what your doing, go for skill for life studies as well.
ReplyDeleteHuyu mzee wa Stanford anavyojitapa!!!hawa ndio wale wazee wa nondozzz na mapicha kedekede hapa globuni hahahahaha....tunakusubiri tuone jinsi ulivyotokelezea baada ya kudaka Ph.D hapa globuni maana kwa staili hii ya maelezo yako lazima tukukoge kwa mapicha ukiwa pamoja na wazungu.
ReplyDeleteHakuna mtu anayeomba wazazi wake wawe maskini hapa duniani.kama umepata bahati ya kufaulu ni kwa uwezo wa MUNGU wala sio ww mwenyewe so angalia sana usijilaani kwa maneno yako wewe braza PhD.
ReplyDeleteMimi nafkiri hii ni siasa tu hapa Tz.tunakosa strategies katika maswala ya muhimu kama haya ya kielimu.hii inatokana na kuongozwa na watu kama huyo wa PhD hapo juu.Serikali inatakiwa kuangaza tena hii sera yake ya elimu kwa wote iko vp??inakidhi mahitaji??inahitaji kuboreshwa???
hivi ni kweli huyu br. anachukua phd?,doubt!;ndg unafikiri kwamba walioko kwenye vyuo vya private walifeli,mbona wapo vijana kibao ambao wametoka shule special ulizozitaja!hili ni swala sensitive sana la kufanyia kazi na serikali,maana baada ya hawa wataalam kihitimu sdhani km huwa kuna tofauti ya degree zao na kazi yao ni ile ya kuokoa maisha ya watu,now why the difference in their sponsorshirp?? plse,naomba wahusika wawajibike!nadhani afya ndo kila kitu kwa maendeleo ya nchi yetu,maana huwezi fanya lolote huku unaumwa.
ReplyDeletePhd!unasikitisha watu elimu bila Mungu ni bure me sipo kwenye hiyo fani but kiukwel they need support .hakuna mtu atakayeamin kwamba wewe ni msomi
ReplyDelete