Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) Unasikitika  kuwaarifu Wakazi wa Jiji na Wananchi kwa jumla kusitishwa huduma treni ya Jiji ( Dar- Ubungo Maziwa) kwa siku ya leo ya Alhamis Oktoba 03, 2013. Hatua hiyo imechukuliwa  kufuatia ajali ya kichwa cha treni hiyo  kugongwa na lori jana Oktoba 2, 2013 saa 12:30 jioni katika makutano ya reli Buguruni. 


Ajali hiyo  imesababisha kuharibika kichwa cha treni na kuhitaji matengenezo kabla ya kuendelea na huduma. Uongozi wa TRL unaahidi kusimamia matengenezo kwa wakati ili huduma za treni za Jiji zirejee mapema kesho Ijumaa Oktoba 04, 2013. Kufuatia ajali hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa zaidi ya lori kupinduka na kuharibika kichwa cha treni.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano , 


Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji  
Mhandisi Kipallo Amani Kisamfu,
Dar es Salaam
Oktoba 03, 2013.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hiki ni kioja cha mwaka,sasa kwanini mnakua na kichwa kimoja tu? Jamani hivi kwa mwendo huu tutafika kweli? Na hiyo mibichwa imepitwa na wakati mtoke nje ya nchi mwende nchi kama vile JAPAN mkajifunze siku hizi mambo yote ni ubunifu wa hali ya juu,mambo ya kisasa,HII NI kalne ya 21 pendezesha jiji la DAR kwa mwendo wa kisasa au mambo ya kisasa,naitwa mdudu kakakuona

    ReplyDelete
  2. kabla ya kwenda Japan kuona mambo ya kisasa inabidi kwanza uende darasani ukajifunze Kiswahili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...