Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga akizungumza juu ya vifurushi vya
Airtel Yatosha Baba lao iliyoboreshwa ili kumuwezesha mteja wa Airtel
kupata dakika 61 kupiga mitandao yote, kutuma ujumbe mfupi wa maneno
bila kikomo pamoja na 1.5GB kwa bei ile ile ya shilingi 999 tu.
Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga akizungumza juu ya vifurushi vya
Airtel Yatosha Baba lao iliyoboreshwa ili kumuwezesha mteja wa Airtel
kupata dakika 61 kupiga mitandao yote, kutuma ujumbe mfupi wa maneno
bila kikomo pamoja na 1.5GB kwa bei ile ile ya shilingi 999 tu.
Mshindi wa nyumba ya tatu ya Airtel
Yatosha, Bi. Husnat Anthony leo amekabidhiwa rasmi cheti chake cha
ushindi ikiwa ni uthibitisho maalum wa ushindi wake .
Mshindi huyo anakuwa ni mshindi wa tatu kuibuka na nyumba kupitia
promosheni ya Airtel yatosha shinda nyumba tatu baada ya nyumba ya
kwanza na ya pili kuchukuliwa na Sylvanus Juma pamoja na Agnes Lyimo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa cheti chake, Bi.
Husnat alisema “Kweli sikutegemea kama ipo siku naweza nikamiliki
nyumba yangu mwenyewe, na hata nilipopigiwa simu sikuamini ila
Namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kuwa mshindi wa nyumba ya Airtel
Yatosha”
“Pia nawashukuru sana Airtel kwa zawadi hii na nimeamini kweli Airtel
yatosha na inasaidia kupunguza makali ya maisha kwa watanzania,”
alisisitiza Bi. Husnat.
Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando alisema
Airtel inayo furaha kumpata mshindi mwingine wa nyumba na haitoacha
kutoa huduma bora na zenye manufaa kwa wateja wake nchi nzima na kwa
sababu hiyo bado inazidi kuboresha huduma zake na kuzifanya ziwe za
kisasa zaidi.
“Airtel hatujaishia tu kwenye utoaji wa nyumba bado tunaendelea
kuboresha huduma zetu na kuhakikisha wateja wetu wananufaika zaidi na
huduma tunazotoa” Alisema Mmbando.
Airtel imeboresha zaidi huduma zake na sasa hivi ukijiunga na
kifurushi cha siku cha 999 unaweza kupata dakika 61, kutuma ujmbe
mfupi wa maneno bila kikomo pamoja na 1.5GB kwa ajili ya matumizi ya
Internet.
Kujiunga na vifurushi mbalimbali vya Airtel mteja anapaswa kupiga
*149*99# na kuchagua 1 au 2 kisha aweze kujiunga na kifurushi chochote
cha Wiki, Siku au Mwenzi.
Airtel kupitia promosheni ya Airtel yatosha imetoa zawadi ya pesa
taslimu shilingi milioni 90 kwa wateja wake na nyumba tatu zenye
thamani ya milioni 65 kwa kila moja tayari zilishapata washindi.


Mtandao wenu sasa hv haufunguki, umekua slow, sijui wateja wamekua wengi au ni nn, angalieni hilo tunawaheshimu sana.
ReplyDelete