Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiwasili katika ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao zilizopo jengo la TTCL mtaa wa Samora leo jijini Dar es salaam kwa lengo la kuangalia shughuli za usimamizi wa mifumo na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika uendeshaji wa shughuli za serikali. 
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na viongozi wa Wakala ya Serikali Mtandao na waandishi wa habari  leo jijini Dar es salaam mara baada ya kupokea taarifa  kuhusu maendeleo ya Tovuti Kuu mpya ya serikali inayosimamiwa na Wakala ya Serikali Mtandao chini ya Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma. Balozi Sefue amefafanua kuwa Tovuti Kuu ya Serikali iliyoanzishwa itawawezesha wananchi kupata taarifa na huduma mbalimbali zinazotolewa na serikali. 
 Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Bakari akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mpango wa serikali katika kuhamasisha na kuendeleza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika shughuli za serikali  kupitia Tovuti Kuu mpya ya serikali iliyoanzishwa  kwa lengo la kuboresha na kurahisisha utoaji wa taarifa na huduma kwa umma, kuhamasisha ushirikishwaji wa raia katika utoaji wa maamuzi yanayowahusu na kuwezesha uwepo wa serikali iliyo wazi.
  Baadhi ya viongozi wa Wakala ya Serikali Mtandao iliyo chini ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na waandishi wa habari wakiwa katika mkutano na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Mwonekano mpya wa Tovuti Kuu ya Serikali ambayo inapatikana katika anuani ya  www.egov.go.tz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kaka Mahumi nakuona hapo. Big Up and Congrats!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...