Operesheni Kimbunga awamu ya Pili
iliyoanza tarehe 21 Septemba, hadi kufikia
tarehe 01 Oktoba, 2013 imekamata watuhumiwa wa ujambazi wa kutumia
silaha 88. Kati ya hawa, 27 walikamatwa mkoani Kigoma, 43 mkoani Geita na 18
mkoani Kagera. Watuhumiwa hawa wanaendelea
kushikiliwa kwa uchunguzi zaidi ili hatimaye wafikishwe kwenye vyombo vya
sheria.
Wakati huo huo, Operesheni hii
imefanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa wa uhamiaji haramu 425, kati yao 166
walikamatwa mkoani Kigoma, 50 mkoani Geita na 209 mkoani Kagera.
Wengine waliokamatwa ni watuhumiwa wa
ujangili 11, kati yao sita mkoani Kigoma na watano mkoani Geita, na watuhumiwa watano
kwa kuhifadhi au kutorosha wahamiaji haramu kati yao wane kutoka mkoa wa Kigoma na mmoja,
mkoa wa Geita.
Vitu vingine vilivyokamatwa katika
Operesheni hii ni SMG 3, Pistol 2 mkoani Kigoma na Gobole 18, moja mkoani
Kigoma na 17 mkoani Geita. Vingine ni risasi 471 za (SMG/SAR), Star Pistol 13,
Magazine za SMG 2, Sare 1 ya Jeshi la Burundi na Shati moja, vyote katika mkoa
wa Kigoma.
Vingine ni bomu moja la kurushwa kwa mkono mkoani Kigoma,
ngombe 2220 katika Hifadhi ya Taifa ya Biharamulo mkoani Kagera, gunia 100 za
mkaa mkoani Geita, gongo lita 271, mkoani Kigoma 11 na 260 mkoani Geita. Nyara za Serikali zilizokamatwa ni ngozi ya
mbweha moja na meno matatu ya Kiboko mkoani Geita. Bangi kilo tatu na nyavu haramu za uvuvi
(makokoro) 12 pia zilikamatwa mkoani Geita.
Akizungumza katika Mkutano na
Waandishi wa habari mjini Bukoba leo, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Simon
Sirro, kwa niaba ya Operesheni Kamanda wa Operesheni Kimbunga, alisema
haieleweki ni vipi watendaji wa Vijiji, Kata na Tarafa wanashindwa kutoa
taarifa kuhusu wahalifu katika maeneo yao, wakiwepo wahamiaji haramu, na kuwa
viongozi hawa wanawajibika na uhalifu unaotokea katika maeneo yao.
Alisema ni imani ya watendaji
wa Operesheni Kimbunga kuwa Watendaji hawa wataanza kuwajibika ili kukomesha
matukio ya uhalifu hapa nchini.
IMEANDALIWA NA TIMU YA HABARI
– OPERESHENI KIMBUNGA
Hizi ofisi zinahitaji kompyuta, bado mnatumia makabrasha peke yake
ReplyDeleteNdugu Zetu Majuu:
ReplyDeleteTanzania imepanda Thamani, Tanzania ya leo sio ile ya miaka kitambo mlipo ondoka.
TANZANIA SASA NI KAMA MAJUU, NA SISI TUNAWATIMUA WAHAMIAJI HARAMU KAMA NINYI MLIVYOKUWA MNATIMULIWA NA KUPELEKWA BENZI NA SERIKALI ZA NCHI ZA HUKO MAJUU!
Huwezi amini Wazungu waliotoka nchi mlizoko huko Majuu nao wamekubmbwa na kulaliwa na hii OPERESHENI KIMBUNGA, zaidi ya hilo hao mnaoona wamekamatwa na kushikiliwa kwa Takwimu hizi hapo juu wengi wao wamezaliwa Tanzania na wamekuwa wakiishi na kujiamini na wengine kijisahau kabisa kama wapo nje ya Sheria ktk suala la Uraia!!!
Hivyo mkitoka huko sijui Sweden, sijui Marekani ama Canada mindhali mlisha ukana Uraia wa Tanzania, mje mkmiwa ndani ya Sheria kamili kwa kuomba Viza kabisa Ubalozi wa Tanzania ktk Maeneo yenu ama Uwanja wa ndege Tanzania na ndio mje na kuingia Tanzania ama sivyo kama hao Wahamiaji Haramu nanyi ni wazi mtamezwa na Mamba kwa kuwa nanyi ''Mtakumbwa na Kimbunga'' !!!
Askari mwanamama aliesimama kifua mmmhhhhhh!!!!!!
ReplyDeleteSasa kwanini hawakamatwi hawa wazembe watendaji wa kata,kijiji,tarafa,wilaya,tumechoka kusikia eti hamjui hawa watendaji wanawajibika kivipi? Ikumbukwe hawa watu wanalipwa mishahara kwahiyo kuwajibika ni lazima wala sio ombi,na mbona hawa wahamiaji HARAMU hawaishi why? Wasakeni nyumba baada ya nyumba,usiku na mchana,poli kwa poli,nimefurahi sn kusikia hiki kimbunga kipo chini ya jeshi letu tukufu la JWTZ mm naliamini sn jeshi langu maana hawanaga mchezo kabisa wakiwa kazini,kwa sasa masikio yangu yapo kwa rais wetu lini atateua kikosi kazi cha JWTZ kulishugulikia tatizo la majangili wa kwenye mbuga zetu za WANYAMA,kama alivyosema hongera sn JK wananchi tupo nyuma yako,
ReplyDeleteSasa huyo mwananchi ni mtuhumiwa au alifika kupata huduma idara ya Uhamiaji/POLISI?
ReplyDeleteMaana hakuna maelezo kuhusu picha ktk mtundiko huu.
Mdau wa Pili,
ReplyDeleteNaungana na wewe ni kuwa ndani ya hao Wahamiaji haramu walio jisahau kumbe wasijue wapo nje ya Sheria za Uraia ingawa walizaliwa Tanzania na kuwa Lugha ya Kiswahili wanaiongea vizuri sana tu, muelewe nanyi kotoka Majuu msifikiri ya kuwa UTANZANIA NI KUWEZA KUJUA LUGHA YA KISWAHILI PEKE YAKE! , LA HIVYO SIVYO UTANZANIA UNAPATIKANA KWA SHERIA NA VIGEZO KAMILI !!!
Majuu mkija Bongo msifikiri Utanzania ni kuwa na babu na bibi ambao bado wapo Tanzania!
ReplyDeleteMsije mkakumbana na Vijana wa Dr.Nchimbi na Kimbunga Chao kwa kuwa tumesha wapa Mamlaka wafanye kazi.