MAREHEMU MZEE ASHERI A.M. MWASANDUBE
Siku, miezi na sasa mwaka mmoja umetimiza tangu Mwenyezi Mungu akuite
nyumbani. Alhamisi ya tarehe 11 Oktoba, 2012 ilikuwa ya majonzi makuu
katika familia yetu, Bwana alipotazama shambani mwake akaona nafasi,
kisha akatazama duniani na kukuona baba yetu mpendwa ukiwa taabani pale
Muhimbili Hospitali, ndipo alipokukumbatia na kukuambia ASHERI Mwanangu
inatosha njoo nyumbani.
Hakika bustani ya Bwana yapendekeza imesheheni watu wake walio bora,
wampendezaye. Nasi tunazidi kumshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha haya,
tangu tulivyokuwa nawe kimwili hadi sasa ambapo unaendelea kudumu nasi
kiroho.
unakumbukwa sana na familia yako Mama ELESIA KATAPA, Watoto wako Hilda,
Sarome, Stephen, Sekela, Abrahamu, wajukuu zako, dada zako, wadogo zako,
ndugu, majirani kila mmoja kwa namna ya pekee.
Kwetu Baba yetu mpendwa unaendelea kudumu katika kila pumzi ya uhai
wetu, tunaendelea kusimama katika misingi uliyoiweka tena bila kutetereka,
tukitumaini kuwa siku moja tutaungana nawe katika kiti cha enzi cha
Bwana wetu Yesu Kristo. "AMEN"
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...