Mshindi  wa kwanza wa mbio za Rock City Marathon 2013 kilomita 21 kwa upande wa wanaume Alphonse Felix kutoka mkoani Arusha akimalizia mbio hizo kwenye uwanja wa CCM Kirumba ambapo alitumia saa 1:02:17 na kufanikiwa kuvunja rekodi iliyowekwa mwaka jana na Opio Chacha aliyetumia saa 1:05:47.
   Afisa Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa hifadhi wa jamii NSSF  Bi. Theopista Mheta akimkabidhi zawadi ya shilingi 1,500,000/= mshindi wa kwanza mbio za Rock City Marathon kilomita 21kwa upande wa wanaume Alphonse Felix ambaye pia alijinyakulia zawadi ya tiketi ya ndege toka moja wa wadhamini wa mbio hizo Precission Air, ya kuelekea Dar es Salaam na kurudi mkoani kwake Arusha.
  Afisa Mauzo wa King’amuzi cha Continental, Dominic Kiluma akikabidhi zawadi ya king’amuzi kwa Joel Kimbiaye toka Kenya mara baada ya kuibuka mshindi wa nafasi ya pili mbio za Rock City Marathon 2013 ambapo pia mshiriki huyo alijinyakulia kitita cha shilingi 900,000/=.
 Afisa Mahusiano na Masoko wa Mfuko wa hifadhi wa jamii NSSF Bi. Theopista Mheta  akikabidhi zawadi ya shilingi 700,000/= mshindi wa tatu katika mbio za Rock City Marathon  kilomita 21, Andrew Sambu ambaye pia alijinyakulia king’amuzi cha Continental.
    Washiriki wa Rock City Marathon 2013 wakichuana vikali kuisaka nafasi za ushindi wa mbio hizo ili kujinyakulia zawadi mbalimbali zilizoanishwa na wadhamini wa michuano hiyo ambao iliandaliwa na ampuni ya Capital Plus International Limited kwa kushirikaina na wadhamini mbalimbali.
Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw, Jackson Mmbando akimpongeza mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita 2, Benedicto Mashauri wa mwanza, baada ya kuwashinda watoto wenzake 284 walioshiriki mbio za Rock City Marathon 2013. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...