Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Bw. Etienne de Poncins, Mkuu wa Chombo kipya chini ya Jumuiya ya Ulaya (EUCAP Nestor) kinachoshughulika na utoaji mafunzo katika masuala ya Usalama Majini kwa nchi za pembe ya Afrika. Bw. Poncins alifika Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha rasmi ombi kwa Serikali ya Tanzania la kujiunga na Chombo hicho ambacho lengo lake kuu ni kutoa mafunzo, misaada ya kiufundi na kisheria ili kuziwezesha nchi washirika kukabiliana na matukio mbalimbali ya Uharamia na Ugaidi yanayotokea katika Bahari Kuu ikiwemo Pwani ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA |
Home
Unlabelled
MHE. MEMBE AKUTANA NA MKUU WA CHOMBO KIPYA CHA EU KUHUSU USALAMA MAJINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...