Shirika la Kimataifa la Mtandao wa Ulaya wa Madeni na Maendeleo, European Network on Debt and Development (Eurodad) watafanya ziara ya kiuchunguzi kuhusu masuala ya uwazi katika kodi katika nchi za Ulaya kuanzia tarehe 20 Oktoba mpaka tarehe 5 Novemba mwaka 2013. Uchunguzi huo utaendeshwa na wataalamu waliobobea wa masuala ya kodi na maendeleo. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali wa Bunge la Tanzania Zitto Zuberi Kabwe ameteuliwa kuongoza Jopo la uchunguzi huo.

Eurodad ni Mtandao wa Mashirika yasiyo ya kiserikali yapatayo 48 kutoka nchi 19 za Ulaya ambayo yanajihusisha na masuala ya kufutia madeni nchi zilizoendelea, misaada yenye maana na kodi za haki. Mashirika haya yamekuwa kwenye kampeni ya kupinga utoroshwaji wa fedha kupitia ukwepaji kodi unaofanywa na mashirika ya kimataifa kwa nchi zinazoendelea. Zitto amekuwa mmoja wa wabunge wanaosimamia hoja ya kutaka Watanzania waliotorosha fedha kwenda nje warejeshe na kufunguliwa mashtaka.

Mwaka 2012 aliwasilisha hoja binafsi Bungeni na kupitishwa kuwa Azimio la Bunge ya kutaka uchunguzi kuhusu utoroshwaji wa fedha na kufichwa nje kama Uswiss. Kikosi Kazi cha Serikali kutekeleza Azimio hilo la Bunge kinatarajia kuwasilisha taarifa yake katika Mkutano wa Kumi na Sita wa Bunge. 

Siku ya Jumatatu tarehe 21 Oktoba Zitto atakutana na Waziri wa Fedha wa Uswiss na maafisa wa mabenki na asasi zisizo za kiserikali zilizopo jijini Geneva. Pia Zitto atahudhuria mkutano wa Kamati ya Kodi ya Umoja wa Mataifa katika kampeni ya kubadili mfumo wa kodi za kimataifa ili kuzuia unyonyaji wa nchi za Kiafrika unaofanywa na Makampuni makubwa ya Kimataifa.

Baada ya Geneva Zitto atatembelea nchi za Luxembourg na Brussels kabla ya kwenda Norway ambapo atamalizia ziara yake kwa Jopo la Wataalamu wa masuala ya kodi na Maendeleo kuandika taarifa maalumu yenye mapendekezo kuhusu kuzuia utoroshaji wa fedha kutoka Afrika.

Zitto atakwenda jijini London kutoa mada kuhusu masuala ya kodi za kimataifa katika mkutano wa Uwazi (Open Government Partnership). Mwenyekiti wa PAC Tanzania atafanya mazungumzo na Mwenyekiti wa PAC Uingereza Bi Margaret Eve Hodge, Lady Hodge MBE, PC, MP kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa mabunge mawili na kuendeleza wito wake kwa makampuni ya kimataifa kulipa kodi zao barani Afrika na kuacha tabia ya kutumia ‘Tax Havens’ kukwepa kodi na kufukarisha nchi za Kiafrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Nchi nyingi zilizoendelea viongozi wake wanajivunia kuona wamewafanyia nini wanachi wao. Viongozi wetu wa kiafrika wanajivunia kuona wamechuma nini kutoka kwa walala hoi.Kiongozi Zitto ni tofauti yuko sawa na viongozi wa mataifa makubwa tofauti na viongozi wetu wa kiafrika.Najivunia Mbunge wangu Zitto tangu akiwa kijana mdogo shuleni alikuwa mfano kwetu.Nimesikitika sana vita ya viongozi kupambana kuficha mishahara kwani hawatendi haki kwa kuwa wanachi ndo waajiri wao kwa hiyo sijui kwa nini wanataka kuwaficha waajiri wao.Heko Zitto keep going tuko pamoja na nchi inakuhitaji sana.wakati unawaandikia umoja wa ulaya kuna waliokubeza ila matokeo tunayaona.

    ReplyDelete
  2. Kila la heri kaka tupo pamoja.

    ReplyDelete
  3. Vizuri Mh. Tunataka uyafanyie kazi mazuri yote utakayo yaona.

    ReplyDelete
  4. Twenze tu

    ReplyDelete
  5. Michuzi, chanzo cha taarifa hii? uwe unaweka source otherwise taarifa rasmi zinaonekana kama za kienyeji tu..

    ReplyDelete
  6. Keep it up Mh.Zito. Watanzania wanakupenda tunajua kuwa kwako ni Tanzania kwanza mengine baadaye.
    MUNGU yuko pamoja na wote wenye mapenzi mema kwa watu wake.
    Atakusaidia tu katika mapambano yako dhidi ya mafisadi wanaowanyonya watanzania.

    ReplyDelete
  7. Tatizo la makampuni makubwa kutokulipa kodi vizuri sio la nchi zinazoendelea tu ni tatizo pia la nchi zilizoendelea pi. Kama unafuatilia vizuri hii ilikuwa pia ni agenda kwenye mkutano wa G8 wa mwaka huu uliyokwisha fanyika.
    Kwahiyo sioni jipya ambalo muheshimiwa Zito ambalo anawezakulifanya. Haya makampuni makubwa yanatumia legal means kukwepa kodi hayafanyi illegal yanauwezo wa kuajili tax consultant ambaye kazi yake ni kupunguza kiasi cha kodi ambayo kampuni inalipa ilikeweza kuongeza utajiri kwa mashare holder wao. Siyo kazi rahisi kama mnavyofikiria kuweza kupambana na haya makampuni kama baadhi ya watu mnavyofikiria ni Global isuue.

    ReplyDelete
  8. Is wake up call for all Tanzania members of government to do what is real benefits of all citizens and by taken Mr Kabwe effort Tanzania in years come will be different nation, with a lot of opportunities for everyone and massive development.
    Good job brother Kabwe all the best, you just announce great movement which describe that Tanzania is not for 1% group of fat individual but for all Tanzania citizens.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...