Ankal salam.
Wasafiri na wasafirishaji katika barabara zetu hupata usumbufu mkubwa sana wanapofika kwenye upimaji wa magari yao katika weigh-bridge (mizani za kupima Magari).
Wenzetu kwenye nchi zilizoendelea wamefikia kuwa na technology ambayo mizani hizo hazina operator (yaani ni unattended).
Yaani dereva akifika katika mizani na truck yake, anaingiza kadi yake kwenye mashine iliyopo hapo (kama tufanyavyo pale airport), halafu gari hupimwa automatically na kumbukumbu zote kuwafikia wahusika kwa mtandao immediately.
Nadhani Tanzania inahitaji mfumo wa kisasa kama huo, ili kuondoa usumbufu uliopo huko kibamba, mikese, Msata, etc.
Eid njema Ankal.
Mdau
Sent from my iPad
Kweli ni wazo zuri sana mdau,tena la kimaendeleo,ila kwa bongo huo usumbufu unauona upo hapo kwa faida ya watu,hawatapenda uondoke maana ni mradi.
ReplyDeleteTanzania kufikia hapo itakuwa ni hatua kubwa sana kimaendeleo.Hivi ni vitu vidogo sana bado vinatushinda.Mbali ya usumbufu wa mizani, foleni za magari kila mahali, barabara finyu na mbovu, njia za mkato zipo lakini ni mbovu na hazipitiki.
ReplyDeleteMizani ijiendeeshayo yenyewe ya kupimia magari.
ReplyDeleteMizani ijiendeeshayo yenyewe ya kupimia magari.
ReplyDeleteJameni mkifunga mitambo hiyo ya kisasa watu 'watakula' wapi?
ReplyDeleteHii pia itaondosha wizi unaofanywa na watendaji walioko kwenye mizani
ReplyDeleteKwenye mizani wanatakiwa labda askari tu lakini mizani ikiungwa na mtandao wa internet hadi kwenye mamlaka wizi wote utaisha, sema tu wabongo tunapenda mno longo longo
ReplyDelete