Mwenyekiti wa Kikao cha kwanza cha Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyokuwa ikihusu Ukubwa wa mifuko ya hifadhi za jamii,Daud Msangi akitoa muongozo kwa Wadau wa PPF waliopo kwenye mkutano huo,kabla ya kumuita mtoa Mada.
Mtoa Mada wa kwanza iliyokuwa ikihusu Ukubwa wa mifuko ya hifadhi za jamii katika Sekta isiyo rasmi, Dominic Muindi ambaye ni Mtaalamu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutoka nchini Kenya akiwasilisha mada yake hiyo kwa Wanachana na Wadau PPF waliopo kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,unaendelea kufanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha leo.
Mchangia Mada iliyokuwa ikihusu Ukubwa wa mifuko ya hifadhi za jamii katika Sekta isiyo rasmi,Dk. Saqware Abdallah Naniyo akifafanua maswala mbali mbali yahusuyo mada hilo iliyowasilishwa na Mtaalamu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutoka nchini Kenya,Ndg. Dominic Muindi katika Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaendelea kufanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha leo.
Mbunge wa Jimbo la Busega,Mh. Titus Kamani akiuliza swali kwa mtoa Mada hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii na Mbunge wa Jimbo la Peramiho,Mh. Jenista Mhagama akichambia mada iliyowasilishwa na Mtaalamu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutoka nchini Kenya,Ndg. Dominic Muindi kutoka nchini Kenya (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,unaendelea kufanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ambaye ni mstaafu wa serikalini,Mzee Samson Kibonde akielezea namna anavyoweza kumudu maisha yake katika mazingira ya ustaafu na kusema amefurahia maisha yake kutokana na kufaidi mafao anayopokea kutoka PPF.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio,Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Dk. Makongoro Mahanga pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii na Mbunge wa Jimbo la Peramiho,Mh. Jenista Mhagama wakifatilia Mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...