Mrembo Happiness Watimanywa akiwashukuru Mkuu wa Mkoa Dr. Nchimbi,wdau wa masuala ya urembo Mkoa wa Dodoma na mashabiki wake wote kwa kumuandalia hafla ya kumpongeza na 'kumsupport' wakati wa mashindano hatimaye kunyakua taji la Redds Miss Tz 2013.
Mkuu wa Mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kushoto) akitoa salamu zake za kumuasa na kumpongeza Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa.
Redds miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa akikata keki tayari kuwalisha wageni waliojitokeza kwenye hafla ya chakula cha jioni ya kumpongeza kushinda taji hilo, hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki kwenye hoteli ya Dodoma.
Mkuu wa Mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwa ameshika kipande cha keki kumlisha Happiness Watimanywa kama ishara ya kumpongeza kwa kushinda taji la Redds Miss Tanzania 2013 akiwa mshiriki kutokea Dodoma kwenye mashindano ya mwaka huu.
Mrembo Happiness Watimanywa wenye meza ya msosi akihudumiwa chakula.
Baadhi ya wadau wa masuala ya urembo, ndugu,jamaa,marafiki na mashabiki wa Mrembo Happiness Watimanywa wakijumuika kwa msosi jioni hiyo.








sasa siyo baadaye ubadilishe jina sijui ujiite nani, hilo Happiness ni jina zuri
ReplyDeletena sio jina tu pekee yake mpaka kitabia, kwa sasa anaonekan msina mzuri na mrembo na mwenye hekima na busara, kwa muonekano tu, lakini binadamu hatabiriki aweza badilika mpakaa.
ReplyDelete