![]() |
Omari Kimweri |
Mpambano huo utakaopigwa nchini China November 30, 2013 Mchina Xiong Zhao Zhong ambaye ni bingwa wa dunia wa WBC ambaye anashikilia taji hilo kwa sasa katika uzito huo
Kimweri anakuwa mtanzania wa kwanza kuwania taji kubwa kabisa Duniani akitokea nchini Austalia.
![]() |
Omari Kimweri na Randy petalcoria |
Kigezo cha kufanya apate pambano hilo kubwa ni kutokana na rekodi yake pamoja na kutakiwa mtu ambaye anatokea bara la Afrika ambapo kura imemdondokea bondia Omari Kimweri, ambapo ni kiu ya mabondia wengi duniani kumiliki mikanda mikubwa ya kimataifa. Kimweri mwenye rekodi ya kucheza michezo 16 ambapo ameshinda michezo 13 na kuchezea kichapo michezo 3 wakati mpinzani wake Xiong Zhao Zhong amecheza michezo 26 akishinda 21 kupigwa 4 na kutoka droo moja.
Mabondia hao wote wana umri wa miaka 31, wakitofautiana kwa mwezi mmoja tu katika kuzaliwa. Mpambano wao umekuwa gumzo katika dunia ambapo kila mmoja anajiandaa kwa nguvu
Kimweri kwa sasa anaefanya mazoezi makali, akipewa sparring na bondia Randy Petalcoria wa Philippines ambaye ni bingwa wa light fly weight.
Omari Kimweri kwa sasa yupo katika mazoezi mazito ya kujiandaa na mpambano huo, akitegemea zaidi dua za Watanzania kwa kuwa ushindi wake ni ushindi wa watanzania wote.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Bondia Omari Kimweri
Ndio yale yale yaliosemwa juzi juzi hapa, watu mnamdandia na kumuita mtanzania, ilhali amechukua uraia wa nchi nyengine. Kwa kuwa tu anafanya jambo la kijivunia kila mmoja anamwita mtanzania, lakini wakati huo huo hamtaki kuwapa uraia wa nchi mbili ha ha ha!!!!!
ReplyDeleteNgojeeni wakati akipanda ulingoni ni muziki wa taifa gani utapigiwa :)