Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia), akihutubia katika mkutano wa jimbo uliofanyika eneo la Lumo, Kata ya Yombo Vituka, Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine alielezea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM jimboni humo.
 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Adam Kimbisa akihutubia katika mkutano wa Jimbo la Temeke eneo la Lumo, Yombo Vituka, Dar es Salaam , ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali kuwajali vijana kwa kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazowakabili. Kutoka kulia ni Mbunge wa jimbo hilo, Abbas Mtemvu, Meya wa Ilala, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Jerry Silaa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu (kushoto),  akihutubia na kummwagia sifa Mbunge wa Jimbo la Temeke, ambaye pia ni Mwenyekiti wa wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu (kulia),  kwa tabia yake ya kuwa karibu na jamii na kutetea maendeleo ya Temeke na Dar es Salaam jana katika mkutano wa jimbo hilo wa kuelezea miradi mbalimbali iliyotekelezwa jimboni humo kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM uliofanyika eneo la Lumo, Kata ya Yombo Vituka, wilayani humo.
 Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile akihutubia katika mkutano huo, ambapo naye alimmwagia sifa Mtemvu na kwamba yupo tayari kufuata nyayo zake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...