Anaitwa Zuriel Oduwole, msichana mdogo wa Kimarekani mwenye asili ya Nigeria, yupo jijini Dar es salaam hivi tunavyoongea akiwa na wazazi wake na wadogo zake watatu, katika harakati zake za kupigia chapuo umuhimu wa kumuendeleza mtoto wa kike katika Afrika. 
Tayari Zuriel ameshafanya mahojiano na Marais wanane (akiwemo Rais Kikwete) pamoja na Waziri Mkuu wanne wa Afrika, pamoja na mfanyabiashara tajiri kuliko wote Afrika Bw. Dangote, hali kadhalika nyota wa tennis duniani toka Marekani, Venus na Serena Williams.
Zuriel, ambaye ni mtengezea filamu, mwanahabari na mwanaharakati wa maslahi ya wasishana wadogo,  yuko nchini akitokea Malawi ambako kama ilivyokuwa hako, hapa nchini, hususan jijini Dar es salaam, atafanya mihadhara katika shule kadhaa ya kuhamasisha wasichana wadogo wajiamini na kusaidia katika kuzungusha gurumu la maendeleo huku wakipiga vita unyanyapaa dhidi yao. Mwezi Agosti mwaka huu Zureil aliweka historia ya kuwa mtu mwenye umri mdogo kuliko wote waliopata kuhojiwa na jarida maarufu la watu maarufu na matajiri duniani la Forbes. VHapideo ya hapo chini kabisa ni moja ya vipindi alivyoandaa:
 Zureil akimhoji Rais wa Liberia Mhe Mama Ellen Johnson Sirleaf
 Zureil akimhoji Rais wa Nigerai Mhe Goodluck Jonathan
 Zureil akimhoji Mhe Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Zureil akimhoji Rais wa Cape Verde Mhe Jorge Carlos Fonseca
Zuriel akiongea na Rais Jakaya Kikwete

Zuriel akimhoji Rais wa Sudan ya Kusini Mhe Salva Kiir Mayardit
Ankal akiwa na familia ya Oduwole na watoto wa marafiki jijini Dar es salaam Jumapili hii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Wapopo wako smart sana upstairs...ni watu wako daring sana

    hapo amewashinda hata wenzangu na mie ambao ni watu wazima lakini kuhoji kiongozi mpaka kigugumizi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...