Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Profesa Elisente Ole Gabriel akizungumza na wanachama wa chama cha waendesha Pikipiki maarufu "Bodaboda" kwenye ukumbi wa Polisi Mess jijini Arusha na kuwataka kujiunga kwa pamoja kukopa fedha za mfuko wa vijana katika halmashauri ya jiji.
Wanachama wa chama cha waendesha Pikipiki jijini Arusha wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo jijini Arusha.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Profesa Elisente Ole Gabriel kushoto akisalimiana na dereva na pikipiki za biashara "bodaboda" baada ya kuzungumza nao ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha vijana kutumia fursa zilizopo kujipatia kipato kwa njia halala na kufata sheria za barabarani.
Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Habari,Vijana,Utamadunu na Michezo,Profesa Elisante Ole Gabriel(katikati) akiwa akiendesha moja ya Pikipiki ya mmoja wa wafanyabiashara wa kubeba abiria jijini Arusha baada ya kuzungumza nao ikiwa ni itimisho la ziara yake ya siku tano mkoa Arusha.
Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Habari,Vijana,Utamadunu na Michezo,Profesa Elisante Ole Gabriel akijaribu kupanda moja ya Pikipiki ya mmoja wa wafanyabiashara wa kubeba abiria jijini Arusha baada ya kuzungumza nao ikiwa ni itimisho la ziara yake ya siku tano mkoa Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Vizuri sana Muheshimiwa Prof. Elisante Ole Gabriel (Naibu Waziri...) - wakati mwingine jambo kama hilo linaweza kukuweka karibu na vijana (wananchi) kwa gharama nafuu sana; nadhani ni mfano mzuri wa kuigwa na viongozi wengine kwa jinsi na namna zao kujaribu kujiweka karibu na wananchi na kutekeleza ahadi & matarajio ya watu wetu - Mungu Ibariki Tanzania!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...