Jamal Emil Malinzi ndiye Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo kwa kupata kura 73 kati ya kura 126 zilizopigwa, dhidi ya mpinzania wake Athumani Nyamlani aliyepata kura 52 kwenye kinyang'anyiro hicho kilichohitimishwa usiku wa kuamkia leo katika jengo la NSSF la Waterfront jijini Dar es salaam.

Malinzi ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha soka cha mkoa wa Kagera ameshinda uchaguzi huo ikiwa ni mara yake ya pili kugombea baada ya kushindwa na Rais wa zamani wa TFF Leodgar Chillah tenga mwaka 2008.Nafasi ya Makamu wa Rais imenyakuliwa na Wallace Kiria aliyemshinda Ramadhani Nasib kwa kura 67 dhidi ya 52, wakati mgombea mwingine katika nafasi hiyo Imani Mahugila Madega kapata kuta 6. 

Katika nafasi za Ujumbe; Kanda ya 13; kiungo wa zamani wa Simba SC Wilfred Kidau amepata kura 60 na kuwashinda Muhsin Said kura 50, Omar Abdulkadir kura 10 na Alex Kabuzelia kura nne. Kanda 12; Khalid Mohamed Abdallah amepata kura 69 na kumshinda Davies  Mosha aliyepata kura 54. 

 Kanda ya 11 Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amepata kura 78 na kuwashinda Riziki Majala kura tano, Twahir Njoki kura mbili, Juma Pinto kura 26 na Farid Mbaraka kura 14, Kanda ya 10 ameshinda Hussein Mwamba aliyepata kura 63, huku Charles Komba akipata nne na Stewart Nasima 58. 

 Kanda ya tisa Othman Kambi aliyepata kura 84 yeye amewashinda Francis Bulame kura 30, wakati James Mhagama aliyepata 93 amemshinda Zafarani Damoda aliyepata kura 11 na Kanda ya nane, Ngube Kiondo amepata kura 73 amemshinda Ayoub Nyaulingo kura 52. 

 Kanda ya Tano, Ahmed Iddi Mgoyi aliyepata kura 92 amemshinda Yussuf Kitumbo aliyepata kura 34, wakati Kanda Omar Walii Ali amepata kura 53 dhidi ya 19 za Ally Mtumwa. 

Eley Mbise amepata kura 51 dhidi ya 53 kura 57 za Lamanda Swai. Mbasha Matutu aliyepata kura 63, amembwaga Vesastis Ligano aliyepata kura 61, wakati Vedastus Lufano aliyepata kura 51, amewashinda Jumbe Odesa Magati kura 11, Mugisha Galibona kura 24 na Samuel Nyalla kura 39 na Kanda namba moja, Karilo Samson hakuwa na mpizani akapita moja kwa moja.
Rais mpya wa TFF Jamal Malinzi akiwa na Dream Team yake baada ya uchaguzi
Rais Mstaafu wa TFF LEodegar Chilla Tenga akimkabidhi mikoba Rais Mpya Jamali Malinzi akkisaidiwa na katibu mkuu Angetille Osiah.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini aliyemaliza muda wake,Leodger Tenga (kushoto) akimkabidhi Mpira Rais Mpya wa shirikisho hilo,Jamal Malinzi mara baada ya kutangazwa mshindi katika Uchaguzi uliofanyika jana na kumalizika usiku wa kuamkia leo,ambapo alimshinda mpinzani wake,Athuman Nyamlani kwa kura 73.uchaguzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Water Front jijini Dar es salaam.Katika uchaguzi huo nafasi ya Umakamu wa Rais ilichukuliwa na Walace Karia ambaye alifanikiwa kuwagaragaraza wapinzani wake Imani Madega na Ramadhan Nassib.
Rais Mpya wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini,Jamal Malinzi akizungumza machache na Wajumbe wa Uchaguzi huo mara baada ya kutangazwa Mshindi wa nafasi ya Urais wa TFF,usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Water Front,jijini Dar es Salaam.Kulia ni Makamu Mpya wa Rais wa TFF,Walace Karia.
Rais Mpya wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini,Jamal Malinzi akipongezana na Makamu Mpya wa Rais wa TFF,Walace Karia mara baada ya kuibuka Kidedea.
Shangwe,Nderemo na Vifijo vilitawala kwenye eneo la Ukumbi wa Water Front jijini Dar es Salaam,mara baada ya Washindi kupatikana.Picha na FullShangwe Blog.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Changamoto! Kutoka kuenguliwa hadi kuwa ndiye Rais wa TFF. Jamal sasa chapa kazi na tekeleza uliyoahidi bila kuleta visingizio. Tenga tunashukuru kwa huduma yako sasa kapumzike. Tutakukumbuka kwa kuweka mfumo wa TFF wenye sura ya Kitaasis.

    ReplyDelete
  2. Nawapongeza viongozi wapya wa TFF waliochaguliwa. Rais Jamal Malizi, Makamu wake W. Kiria na wajumbe wote.

    Pia nawapongeza viongozi waliomaliza muda wao L. Tenga & wenzie kwa kazi nzuri. Najua pamoja na changamoto mbalimbali mmeweza kutoa mchango wenu kiasi fulani katika soka letu....najua nyie siyo malaika na hivyo kuna maeneo hamkuweza kufanya vizuri kiasi cha kuridhisha sana lakini hii haiondoi ukweli kuwa angalau mliweza kuifikisha TFF katika nafasi ya kuwa taasisi iliyojipambanua kimuundo na kutoa nafasi sasa ya kuufanyia kazi muudo huu uliopo na kuboresha kama iko haja.

    Kwako Ndugu Rais unayeingia madarakani: Jitahidi kuanza kazi kwa ku-address makundi yaliyojitokeza wakati wa mchakato wa uchaguzi kabla na baada ya rufaa zile zilizokatwa na hatimaye kutufikisha hapa tulipo leo.

    Kusiwepo tena sababu ya kunyosheana vidole ikiwa sasa ni wakati wakujenga soka letu basi Ndg. Malinzi ujue kuwa unawahitaji wadau wote wakiwemo viongozi waliomaliza muda wao. Usisite kuwatumia ukiona iko haja; kumbuka wao hawawezi kukuomba ili wakupe ushirikiano bali ni wajibu wako kuona wewe unawaweka karibu ili uongozi wako uwe mwepesi maana kumbuka wakati wote nguvu yako iko kwa muitikio wa wadau wote wa soka.

    Ndg. Rais (Malinzi), Ukifanikiwa kuwa mnyenyekevu kidogo tu,ukaheshimu kuwa hata L. Tenga ni mdau wa muhimu sana katika kufanikisha kipindi cha uongozi wako wa u-Rais wa TFF utajikuta na wote wanaomuheshimu Tenga (kama Rais aliyemaliza muda wake)utakuwa umewapata.

    Kumbuka kuthamini walichofanya watangulizi wako, utafanikiwa sana katika uongozi wako. Nataka nikwambie hata akina Mzee Ndolanga kwako ni watu wa muhimu - Usiache kutumia uzoefu wao. Utafanikiwa sana maana hata Mzee Ndolanga naye anao watu nyuma yake na hivyo ukimpata Ndolanga (kama mdau wa muhimu katika soka) utakuwa pia umewapata wote wanaomuheshimu Ndolanga. Jitahidi kufanya hivyo kwa wengine wote unaowajua kama wadau wakuu wa soka waliokutangulia - utafanikiwa sana katika uongozi wako.

    Jambo la mwisho ni hili: Ndg. Rais wewe ndiyo mwenye dhamana ya kutekeleza katiba ya TFF kwahiyo kila ambalo TFF itafanya tangu sasa iwe mafanikio au kukosea ni wewe utakuwa unawajibika. Hivyo hata ukiweza kuwatumia vizuri wadao mbalimbali wa soka mwisho wa siku sifa na heshima zitakuwa ni kwako na kipindi chako cha uongozi. Jitahidi kuwa mnyenyekevu ukijitahidi kuondoa malumbano wewe ni tayari Rais wa TFF hakuna haja ya visasi wala bifu na mtu yeyote tumia nguv u nyingi kufanya kazi kuliko kuendeleza visasi maana itakupotezea muda - Ni mtazamo binafsi ila ni maonyo pia kwa uongozi mpya ili waweze kufanikiwa!

    ReplyDelete
  3. Hongera sana Rais wetu mpya Jamal Malizi pomoja ya safu yako ya uongozi!

    Kwakuwa huko nyuma kulikuwa na changamoto nyingi kabla hujafikia hatua hii ya sasa unahitaji kuwa na hekima ya ziada ili kendesha TFF ukiwashirikisha wadau wote.

    Ukiweza "at least kuwa humbled" na kuanza utendaji wako wa kazi ya Rais wa TFF kama "taxi driver" utafanikiwa sana, kwanini? kwasababu kwa taxi driver "wote ni abiria wangu" hata kama jana mama nanihi alinyimwa chumvi alipoenda kuomba kwa jirani haina maana kuwa huyo jirani yako hatakuwa abiria wako kwa sababu hiyo.

    Hakikisha unaiunganisha TFF maana wewe ndiyo rais wetu .... na wote ni abiria wako, hata kama huko nyuma mliwahi kutofautian kimtazamo & kiitikadi!

    Kila la heri Ndg. Rais J. Malinzi. Usiwasahau wazee & waliokutangulia maana hii TFF uliyoikuta sasa wako amba kwa kiasi chao waliweza kuijenga hiyo taasisi. Hata kama walikuwa na mapungufu katka maeneo fulani bado wao ni watu wa muhimu kukupa msaada ili uongozi wako ufanikiwe - Tutafakari kwa Pamoja!

    ReplyDelete
  4. Historia iliyowaweka Vingozi madarakani iwekwe pembeni, wanatakiwa wawe wepesi wa kuona , kutekeleza na kukabiliana na majukumu na changamoto mbalimbali vinginevyo wataona muda wa kukaa madarakani ni mfupi na hawatatekeleza majukumu yao. Wasitumie muda wao kunanga uongozi uliopita, wala kujifananisha bali wafanye na watanzania wahesabu yaliyofanyika.
    Tunawapongeza na tunawatakia mema.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...