Na Ripota wa Globu ya Jamii, Nairobi
Mheshimiwa Prof. Mark J. Mwandosya(MB), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi Maalum yuko katika ziara ya kikazi hapa Nairobi kuanzia tarehe 7 Oktoba, 2013 akiongoza ujumbe wa watu sita kutoka Taasisi mbalimbali za Udhibiti.
Akiwa hapa Nairobi, Mheshimiwa Waziri Mwandosya atatembelea Wizara na Taasisi zinazujishughulisha na Udhibiti wa huduma katika sekta za umeme, maji, ‘gesi, mwawasiliano, usafiri wa anga, majini na nchi kavu pamoja na Taasisi ya Uwekezaji ya Kenya.
Katika siku yake ya kwanza ya ziara yake tarehe 7 Oktoba, 2013, Mheshimiwa Mwandosya na Ujumbe wake alikutana na uongozi wa Maalaka ya Uwekezaji wa Kenya (Kenya Investment Authority), ukiongozwa na Dkt. Moses Ikiara, Managing director.
Pia alikutana na Mheshimiwa Dkt. Fred Matiangi, Waziri wa Mawasiliano wa Kenya. Mheshimiwa Waziri Mwandosya leo atakutana na uongozi wa Energy Regulatory Commission, Communication Commission of Kenya (CCK), pamoja na National Communication Secretariat
Profesa Mwandosya akipata ufafanuzi kutoka kwa Dkt. Moses Ikiara, MD wa Kenya Investiment Authority kuhusu utendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji, changamoto zilizopo na mwelekeo wa baadaye wa mamlaka hiyo
Profesa Mwandosya akimkabidhi kitabu shake Dkt. Moses Ikiara, MD wa Kenya Investiment Authority
![]() |
| Profesa Mwandosya katika Picha ya pamoja na timu ya Uongozi ya malaka ya Uwekezaji Kenya pamoja na ujumbe wake alioongozana nao. |






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...