Na Mwandishi watu, Dar es Salaam
Rais Jakaya Kikwete anatarajia kufungua rasmi kambi ya kwanza ya vijana katika kilimo na maarifa ya Mkongo iliyo katika wilaya ya Rufiji mkoani Pwani Jumamosi wiki hii.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji Bonde la Mto Rufiji (RUBADA), Bw. Aloyce Masanja ambao ndio waanzilishi wa kambi hiyo, uanzishwaji wa kambi hiyo ni moja ya utekelezaji wa kuwashirikisha vijana kwenye kilimo.
“Mpango huu ni sehemu ya utekelezaji wa mageuzi katika sekta ya kilimo wenye lengo la kuwabadilisha kimtazamo vijana ili kukubali na kuona kuwa kilimo kinalipa,” aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.
Bw. Masanja alisema kuwa mpango huu unawajengea uwezo vijana ili waweze kushiriki ipasavyo kwenye shughuli za kilimo na unalenga katika maeneo yaliyochaguliwa kwa ajili ya Matokeo Makubwa Sasa kwenye bonde la mto Rufiji.
Pia alisema ni utekelezaji wa mpango wa kukuza kilimo katika ukanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT) ambao unalenga kuleta mapinduzi ya haraka ya kilimo kikanda unaojumuisha jitihada na nguvu za pamoja za wadau mbalimbali.
RUBADA inatekeleza mpango huu kwa mtindo wa “Hub and Spoke” ambapo mwekezaji mkubwa wa ndani au wa nje anakuwa “Hub” na wakulima wadogo wanakuwa “Spoke” wote kwa pamoja wakisukuma gurudumu la maendeleo.
Akifafanua zaidi alisema mtindo huu unahusu kuanzisha kambi za vijana kwa kila eneo lenye mwekezaji mkubwa katika bonde zima la mto Rufiji linaloanzia mkoa wa Pwani, Morogoro, Iringa, Mbeya, sehemu ya Dodoma, Singida, Ruvuma na Lindi.
Bw. Masanja alisema kufuatana na mkakati sa SAGCOT uliobainisha kongani sita za Rufiji, Kilombero, Ihemi, Mbarali, Ludewa na Sumbawanga; RUBADA, imeandaa mpango kabambe wa utekelezaji ambao utashirikisha vijana katika kila kongani.
“Kwa mwaka huu wa fedha, tunategemea kuwa na vituo vitano vya vijana katika kilimo na maarifa na kila kituo kitakuwa na vijana wasiopungua 300 ambao watapata mafunzo katika kipindi cha mwaka mmoja,” alisema.
Vituo hivyo vya vijana vitakuwa na majukumu ya kutoa mafunzo kuhusiana na utekelezaji wa kilimo bora chenye tija; kuongeza thamani mazao; matumizi ya vifaa vya kisasa; utekelezaji wa kilimo bora bila uharibifu wa mazingira; kuandaa andiko la mradi ili kuweza kupata mikopo katika taasisi za fedha na uundaji wa vikundi vya ushirika.
Kwa mujibu wa Bw. Masanja, mafunzo katika kambi hizo yatajikita katika maeneo makuu matatu yakihusisha uzalishaji wa mazo ya kilimo kwa wingi na yenye thamani kubwa hasa mazao ya bustani, mboga mboga na matunda; ufugaji wa kisasa wa ng’ombe na kuku na ufugaji wa samaki pamoja na ujasiriamali.
Kwa kuanzia, kambi ya Mkongo inaanza na vijana 50 lakini ikiwa na lengo la kuchukua vijana 300 kwa mara moja ili kituo kiweze kufikia malengo yake.
“RUBADA inatarajia kuzalisha vijana 600 kutoka kituo cha Mkongo hadi 2015 ambao watakuwa na utaalamu na ujuzi wa kilimo chenye tija na ufugaji wa kisasa,” alisema Mkurugenzi huyo.
Kilimo ni moja ya sekta zinazolengwa katika mikakati mbalimbali ya serikali katika mapinduzi ya kiuchumi na kufikia malengo ya Milenia na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025.
Kulingana na sense ya watu ya 2012, asilimia 60 ya nguvu kazi ya Tanzania ni vijana.
Kilimo kama Ajira na Ujasiriamali wa Kisasa.
ReplyDeleteHongera Mhe. Raisi kwa Economic Transformation kubwa kama hii na hasa kuwashirikisha vijana ktk Kilimo cha Kisasa.
Kwa hatua hii ni muhimu:
1.Kilimo kikachukuliwa kama Ajira na Ujasiriamali wa Kisasa ili kuwavuta vijana kwa wingi na kuwapa utayari wa kukipokea.
2.Ile dhana ya Kilimo kama fani ya Mzee Jangala iondolewe akilini mwa vishoka wa mazao ya wakulima ambao wamekuwa wakijinufaisha na kuwadidimiza wakulima hadi Kilimo ikawa ni mateso na si fani ama sekta ya Kiuchumi.
3.Ni muhimu Mfumo wa Masoko ya bidhaa za Kilimo ukabadilishwa na kuboreshwa ikiwezekana kuwaondoa Madalali wa mazao ya wakulima na Vyama vya Ushirika nyonyaji vilivyo wadidimiza wakulima kwa miaka mingi sasa, pia Halmashauri nyonyaji zinatakiwa zipewe mwelekeo na mashariti mapya ya Uwakala wa kununua mazao ya wakulima ili wakulima wanufaike na waone kama Kilimo sio fani ya mzee Jangala bali ni Ajira na Ujasiriamali wa Kisasa kwa SURA MPYA YA TIJA NA MAENDELEO.
4.Kilimo kiwe ni cha Kisasa kwa matumizi ya Sayansi na Tekinolojia kwa vifaa badala ya majembe ya mikono na matarajio ya kuvuna kwa kujikimu kwa chakula cha kifamilia tu.
5.Uwezeshaji wa Kifedha uwepo kwa Mabenki na Taasisi za Mitaji kuwadhamini wakulima, pia Kilimo kisiwe cha (i)Kuzalisha mali ghafi, tu bali mavuno yaongezwe thamani na kuongeza ajira (ii)Kilimo kisitegemee asilia pekee bali Sayansi na Tekinolojia itumike kwa mbegu bora zinazotoa mazao zaidi, zinazohimili ukame kuepukana na athari za Mabadiliko ya hali ya hewa Duniani, zinazo himili magonjwa na Kuacha kutegemea misimu ya mvua kwa kumwagilia mazao mashambani.
KWA HAYO MATANO (5) NADHANI KAZI YA UMACHINGA MIJINI KWA VIJANA HAUTALIPA ZAIDI YA KILIMO HIVYO VIJANA WATATIMKIA KWENYE MIRADI YA RUBADA KAMA HUKO RUFIJI NA KWINGINEKO ITAKAKAKO ANZISHWA.
Ni mpango mzuri sana lakini hebu tufikie mahali sasa tuone hivi vitu vinavyo anzishwa kwa ushuhuda wa viondozi wakubwa vina simamiwa na watanzania wanapata mrejesho wa mambo haya ili kuweza kuwavutia vijana zaidi katika kilimo. Kwa mfano tungependa kusikia ule mradi ulioanzishwa coast region na Mh Mwantumu Mahiza umefikia wapi na maendeleo yake yakoje, challenges ni zipi ili tujivunie kilicho chetu!
ReplyDeleteVilevile nitoe rai kwa dau wa kilimo kutembelea ofisi za Private Agricultural Sector Support (PASS) ambazo zipo katika kanda zote nchini: Morogoro (Kanda ya Mashariki); Mbeya (Madgaribi) Mwanza Lake zone); Kilimanjaro (Kaskazini) Mtwara (Kusini) ili waweze kuunganishwa na huduma za kifedha kwa secta ya Kilimo