Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya
afya (NHIF) mkoa wa Iringa Emmanuel W. Mwikwabe akieleza faida ya
TIKA mbele ya washiriki
Sekretarieti ya NHIF
Meza kuu ikifuatilia warsha ya mfuko wa Afya ya jamii mijini (TIKA) leo
Mwakilishi kutoka TAMISEMI Edwin Mgendera mkurugenzi msaidizi idara ya huduma na sheria akijitambulisha rasmi
Mkuu wa mkoa wa Njombe Bw Msangi katikati akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali.makundi mbali mbali ya washiriki.
Meneja wa CHF kutoka NHIF Bw Constantine Anthon Maleda akitoa mada juu ya TIKA
Na FrancisGodwinBlog,Njombe
Meneja wa CHF kutoka NHIF Bw Constantine Anthon Maleda akitoa mada juu ya TIKA
Na FrancisGodwinBlog,Njombe
serikali ya mkoa wa
Njombe iimewataka wanasiasa
katika mkoa huo kuendelea
kuhamasisha wananchi kujiunga na
mfuko wa afya
ya jamii (CHF) unaowalenga wananchi
wa vijijini na ule wa tiba kwa kadi (TIKA) kwa mijini.
Mkuu wa mkoa
wa Njombe kepteni mstaafu Asseri
Msangi alitoa ratiba hiyo
mara baada ya kufungua warsha warsha
ya uanzishaji wa mfuko wa
afya ya jamii mijii (TIKA) katika mji wa
Makambako mkoani Njombe kwenye ukumbi wa RC mjini Makambako mkoa wa Njombe leo
Alisema kuwa serikali
kjupitia wizara ya afya
na ustawi wa jamii imeandaa mfumo huo wa tiba kwa jamii ili
kuisaidia jamii kuweza
kupata matibabu pale inapopatwa
na matatizo ya kifya na kuwa katuka nchi zote
duniani hakuna nchi hata moja ambayo inatoa bure huduma za afya kwa wananchi
wake ukiacha nchi ya Libya ambayo
ilikuwa ikitoa bure matibabu ila
kwa sasa huduma hiyo katika nchi hiyo pia haipo.
Hata hivyo mkuu huyo wa
mkoa aliwataka madiwani katika
kuweka usawa mzuri katika
uchangiaji wa huduma
za afya kupitia huduma hiyo
tiba kwa kadi ili kuwawezesha
wananchi wengi kujiunga na mpango huo.
Kaimu meneja wa mfuko wa Taifa wa
bima ya afya (NHIF) mkoa wa Iringa Emmanuel W. Mwikwabe akielezea
juu ya makusanyo ya NHIF katika mkoa wa Njombe alisema kuwa kwa
mwaka 2012/2013 kiasi cha Tsh milioni 428 zimekusanywa katika wilaya
ya Makete ,Njombe mji na Halmashauri ya wilaya ya Njombe pamoja na
Ludewa.
Alisema kuwa fedha hizo ni makusanyo
ya mfuko wa NHIF na CHF ambapo katika wilaya ya Makete jumla ya
Tsh milioni 70.2 za NHIF zilikusanywa na Tsh milioni 28 za CHF
zilikusanywa na kufanya jumla kuu kwa wilaya hiyo kufikia Tsh
milioni 98.2.
Wakati wilaya ya Ludewa makusanyo ya
NHIF ilikuwa ni Tsh miliioni 78 na CHF ilikuwa ni Tsh milioni 47 na
kufikisha jumla ya Tsh milioni 125 na wilaya ya Njombe mji makusanyo
ya CHF ilikuwa ni milioni 1 na NHIF ilikuwa ni kiasi cha Tsh. milioni
94.8 na Halmashauri ya Njombe fedha za CHF ni Tsh.milioni 2 na NHIF
ilikuwa Tsh.milioni 106.9
Hivyo alisema kumekuwepo na mwitikio
mkubwa wa wananchi kujiunga na mifuko ya CHF na NHIF hivyo ni imani
yake iwapo uhamasishaji utafanyika vema kwa mfuko huo wa TIKA pia
wananchi wengi watajiunga na kunufaika zaidi.
Alizitaka Halmashauri kuwa na
mikamkati ya kuboresha huduma ya upatikanaji wa dawa ,vifaa tiba
,uhusiano mzuri kati ya watoa huduma na wagonjwa ili asilimia 30
ya Halmashauri ziwe na mikakati na mbinu endelevu ya uhamasishaji
inayoshirikisha jamii kwa ujumla.
Meneja huyo alisema kuwa fedha za
makusanyo yatokanayo na CHF na NHIF asilimia 2 ya 3 kununua dawa na
usimamizi wa upatikanaji na matumizi ya dawa (CHMT's)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...