Serikali imesema itaendelea kujikita katika kuwezesha sekta binafsi kuchangia kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2013/2014 ili kuchagiza ukuaji wa haraka wa uchumi wa nchi.

Hayo yaliwekwa bayana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Joyce Mkinga alipokuwa akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari jana katika ukumbi wa Maelezo jijini Dar es Salaam.

Bibi Mkinga alisema kuwa katika kufikia lengo hili serikali imedhamiria kuongeza mikopo kwa sekta binafsi kufikia asilimia 20.0 ya Pato la Taifa kufikia Juni 2014 ili kuwezesha sekta binafsi kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa na kushiriki shughuli nyingine za kimaendeleo.

“Katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2013/14 Serikali inatilia mkazo ushiriki wa sekta binafsi katika uwekezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo Serikali inaendelea kuweka mazingira mazuri ya biashara na kuiwezesha sekta binafsi iweze kukopa kwa ajili ya kuwekeza katika maendeleo ya nchi,” alisema.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Joyce Mkinga akiwaonesha wanahabari Nyaraka ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka 2011 – 2016 apokuwa akizungumza nao katika ukumbi wa Maelezo jijini Dar es Salaam.
Mchumi Mwandamizi toka Ofisi ya Rais, Tume ya MipangoBw. Andrea Aloyce (Kushoto) akifanunua juu ya Sheria ya Ushirikiano kati ya Sekta Umma na Sekta Binafsi (PPP). Katikati ni Bibi Joyce Mkinga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Kulia ni Bi Fatma Salum wa Idara ya Habari. alipokuwa akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari jana katika ukumbi wa Maelezo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...