Sensei Rumadha Fundi mtanzania mtaalamu wa mchezo wa karate mwenye
mkanda mweusi na dan 3 siku ya 12.10.2013 hadi 13.10.2013 aliongoza
semina ya mazoezi ya kata za karate za mtindo wa Goju Ryu
huko Texas,Marekeni,ambako semina hiyo iliudhuriwa na wataalamu na
walimu mbali mbali wa Karate.
Sensei Rumadha Fundi ambaye pia
ni mwalimu wa Yoga ni mmoja ya wataalamu wachache sana wa kiafrika
wenye uwezo wa juu na kukubalika kimataifa,mtaalamu huyu mtanzania
alipata mafunzo yake ya juu kule Okinawa,Japani.pia alisomea mambo
ya Yoga nchini India.Sensei Rumadha Fundi pia ana shahada ya tiba,
utibabu wa mapafu na moyo.Watanzania wana kila sababu ya kujivunia
mtoto wao Sensei Rumadha Fundi kutoka Uswahilini hadi ughaibuni.
Sensei Rumadha Fundi, Mtaalamu wa Karate mwenye dan tatu au (Sandan), katika mazoezi ya Kata ya ngazi za juu za mtindo wa Goju Ryu inaitwa "TENSHO", ambayo hii ndio ilikuwa semina ya kuweza kumudu (kupiga msasa) kata za ngazi ya juu ya Okinawa Goju ryu Karate-Do. Pia semina hiyo ilihusisha katas nyingine kama vile : Geki sa dai ichi; Geki sai da ni; Saifa;Shison chin; Sanseru;Sepai; Kururunfa, Tensho, na Sanchin.
Katika picha, Sensei Rumadha na wenzie katika zoezi la kata ya "Tensho" jana octoba 12, 2013 huko Mesquite, Texas.
Sensei Rumadha Fundi akitoa mafunzo ya kata za karate za mtindo wa Goju Ryu huko Texas,Marekeni
Sensei Rumadha Fundi (shoto) akiwa katika picha ya pamoja na Masensei wenzake waliokuwa wakihudhulia Semina hiyo huko,Texas,Marekeni.
Sensei Rumadha Fundi (shoto) akiongoza safu ya mafunzo ya kata za karate za mtindo wa Goju Ryu huko Texas,Marekeni
Sensei Rumadha Fundi (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Masensei wenzake waliokuwa wakihudhulia Semina hiyo huko,Texas,Marekeni.
Mchezo ukiendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...