JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
SOMO MUHIMU KWA WADAU
ASIYE RAIA WA
TANZANIA NI NANI?
Maswali mengi yanaulizwa kuhusu uraia, hasa wakati
huu ambapo zoezi la kuwabaini wageni wanaoishi nchini kinyume cha sheria
linaendelea katika maeneo mbalimbali nchini, yakitaka kujua nani hasa ni raia
wa Tanzania.
Kimsingi, masuala ya
uraia duniani kote yanaongozwa na falsafa kuu mbili ambazo ni Haki za Kidamu (Jus
Sanguinis - The rights of blood),
ambapo mtu hupata uraia kutokana na uhusiano wa kidamu na wazazi
wenye uraia wa nchi husika. Hii ina maana kwamba, pamoja na mtu kuzaliwa katika
nchi husika anatakiwa pia kuwa na mzazi ambaye ni raia wa nchi hiyo. Falsafa
hii ndiyo inayofuatwa na nchi ya Tanzania.
Kwa maana nyingine
kuzaliwa pekee nchini Tanzania hakumpi mtu haki ya moja kwa moja ya kuwa raia wa Tanzania, bali mtu atakuwa raia
ikiwa amezaliwa Tanzania na wakati wa kuzaliwa kwake mzazi wake mmoja sharti
awe ni raia wa Tanzania.
Falsafa nyingine ni (Jus
Soli - The right of Soil), ambayo mtu
hupata Uraia kutokana na kuzaliwa kwake katika ardhi ya nchi fulani.
Kufuatana na Falsafa hii, mtu hupata uraia kutokana na kuzaliwa katika nchi
husika bila kujali uraia wa wazazi wake.
URAIA WA TANZANIA
Masuala ya uraia nchini
Tanzania yanasimamiwa na Sheria ya Uraia ya Tanzania ya mwaka 1995 Sura 357
kama ilivyorejewa mwaka 2002, pamoja na kanuni zake za mwaka 1997. Sheria
hii imeanisha aina tatu za uraia wa Tanzania ambazo ni;
1.
Uraia wa Tanzania kwa kuzaliwa
2.
Uraia wa Tanzania kwa kurithi
3.
Uraia wa Tanzania kwa Tajnisi, au kujiandikisha.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Hakuna hata nchi moja duniani ambayo iliwahi kuruhusu uraia wa nchi mbili na baada ya muda ikabatilisha. Kuna nchi nyingi duniani ambazo awali zilizuia uraia wa nchi mbili na sasa zinaruhusu uraia wa nchi mbili.
ReplyDeleteTanzania iko siku nayo itaruhusu uraia wa nchi mbili. Anaebisha na akumbushwe (kama ni mdogo) au akumbuke huko nyumba Tanzania ikiongozwa na JK Nyerer ilikataa kata kata kuwa nchi ya vyama vya siasa lakini mwisho JK Nyerere mwenyewe alikuja kubali kuwa wakati umefika wa kuwa na multi party.
Wengi wanaopinga kuwepo kwa uraia wa nchi mbili hawana sababu za msingi zaidi ya uchoyo na wivu, pia kuwa na dhana ya kuwa alie nje ya nchi na ambae ana passport ya nchi nyengine basi atakuwa alijifanya mkimbizi na ameukana uraia wa Tanzania.
Ukweli ni kuwa kuna watanzania tele nchi za nje ambao wana passport za kigeni na wamezipata bila kujifanya wakimbizi wa kisiasa kutoka somali na kwengineko. Ukiangalia passport zao zinasema wazi kuwa mahali pa kuzaliwa ni Tanzania. Hawa hawakuukataa uraia wao wa Tanzani.
Wale ambao wamepata passport za nchi za kigeni kwa kujifanya wakimbizi wa kisiasa kutoka somali na kwengineko, passport zao zinasema wazi kuwa ni wazawa wa nchi walizodai wanatokea, hawa wameukataa uraia wao wa Tanzania, na hawastahiki kuendelea kuwa raia wa Tanzania.
Kampeni ya kuwa na uraia wa nchi mbili unaopiganiwa ni wa hawa ambao ingawa wana passport za kigeni lakini hawakujifanya wakimbi kutoka nje nyengine na passport zao zinasema kuwa wao ni wazawa wa Tanzania.
Mkulima
URAIA:
ReplyDeleteKiendawili hicho hapo juu kazi tunayo!
Je, Mkubwa hivi kama Uraia unaambulika kwa Vigezo vya Unasaba yaani Damu au DNA, kweli Maabara zetu zinao uwezo wa kubeba tathimini hiyo?
Isije fanyika Vipimo halafu mtu akajikuta anatupwa nje ya Utanzania kwa Kigezo cha Vipimo vya Kimakosa vya Unasaba !!!
Vigezo hivyo Vitatu
ReplyDelete1.Uaria wa Kuzaliwa
2.Uraia wa Kurithi
3.Uraia wa Tajnisi au Kuandikishwa,
Vyooote vimekaa Kimtego, tusije kukatumia Siasa kuenguana kwa kuchezesha hivyo Vigezo vitatu na kuweza kumtoa mtu kafara!!!
Je Bwana Mkubwa moa Makala hii, pana uhakika gani watu wakakaguliwa uhalali wa Uraia wao kwa vigezo hivyo vitatu No.1 ,No.2 na No.3 ?
ReplyDeleteHili tangazo kwa kweli limenishtua sana...sikuwa najua kwamba Tanzania Ina sheria za uraia za kizamani namna hii. Kwenye mataifa makubwa, mfano Marekani, ukizaliwa katika nchi hiyo wewe ni raia wao bila kujali Kama mmoja wa wazazi wako ni Mmarekani au vipi. Ninaamini hii ni sababu mojawapo iliyoifanya Marekani kuwa taifa kubwa Kama lilivyo sasa. Sisi nchi yetu ni masikini wa kutupwa na bado tunabagua nani awe raia na nani asiwe raia! This is a shame...na sijui hawa waliotunga sheria hii walikuwa na maana gani maana ukianza kuchunguza nani ni raia na nani si raia, utakuja kugundua kuwa asilimia kubwa ya watu wanaojiita ni Watanzania si Watanzania kwa sababu tu wazazi wao hawakuwa raia wa Tanzania. Hii Tume ya Marekebisho ya Katiba haina budi kuliangalia suala hili na kulifanyia marekebisho kwa faida ya nchi yeti kwa ujumla.
ReplyDeleteMhhhh!
ReplyDeleteAnkali Michuzi kwa Mashariti hayo hapo matatu 'magumu' ya Uraia wa Tanzania hata wewe mwenywe Mjomba Michuzi unaweza kujikuta ni Mgeni hapa Tanzania !!!
Usije kuwa mbogo licha ya kukaa kwako sana Bongo utakataa ukiitwa Banyamulenge?
Usije kufikiri kuwa Mwana Yanga na kuwa Mwana CCM ndio utaupata Utanzania!
Hahahahaha!!!
ReplyDeleteWatoa Maoni wa 1 hadi wa 6 wamenivunja mbavu zangu!
Kubwa zaidi ni huyo No.6 hapo juu akisema kwa 'mashariti magumu ya Uraia wa Tanzania' hata Ankali Michuzi atakuwa Mgeni nchini licha ya kuwa Mwana Yanga na Mwana CCM !