Sr Consolata Shayo 30 Mei 1935 – 15 Oktoba 2013

Mama mlezi, Mkuu wa Shule ya Wasichana Kibosho Sekondari kwa muda mrefu sana kuanzia miaka ya 1960 mpaka 1990. Mama, umetulea, umetutunza, umetujengea uwezo, umetuonyesha njia ya maisha bora. Sasa siku nyingine imefika, tuko hapa peke yetu, tumebaki na masikitiko, haupo tena na sisi. Ulikuwa mara nyingi ukisema kwaheri, na wengine tulikuuliza kwa nini? Kweli sasa umeondoka na kutuacha na mstuko. Machozi yanatutoka katika hali ya kibinadamu lakini tunashukuru, mapenzi ya Mungu yatimizwe.

Hata hivyo tunafarijika tukifikiri kuwa, kwa kazi kubwa uliyofanya duniani, ikatoa wanawake jasiri kama sisi, sasa upo katika pumziko la milele na Mungu na Malaika wa Mbinguni. Kimwili umetutoka, lakini kiroho bado upo hai katika kumbukumbu zetu.

Katika hali hii, hatujabaki peke yetu, bado upo mama. Ingawa uko mbali na macho yetu, kumbukumbu yako bado inaishi. Tulibarikiwa sana na tunamshukuru Mungu kwani alitupa bahati ya kulelewa na wewe mama Consolata na kutokana na malezi yako tumejifunza jinsi ya kuwa mfano bora wa mama. Watoto wetu wanafaidi malezi yako, na tunaamini watayapeleka kwa wana wao hivyo kwa jinsi hiyo kumbukumbu yako itaendelea kuishi na kutoa Baraka vizazi hata vizazi. Mama,kwaheri. Tunakuombea Mola akupe mapumziko mema. Amen!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Dr. Ave MariaOctober 17, 2013

    Mother tuko hapa tulipo kwa kupitia mikono yako. Mother ulitupenda, ulitulea, ulitusindikiza katika njia ya mafanikio. RIP mother Consolata
    Dr. Ave Maria Semakafu

    ReplyDelete
  2. Mama yetu mpendwa hatutakusahau katika maisha yetu mafanikio yetu ni wewe Mama yetu mpendwa ulitufundisha mengi sana ambayo hayaelezeki. Tuko pamoja na familia katika kipindi hiki cha huzuni.

    ReplyDelete
  3. Jamani, Mother Conso,hatuna jinsi ya kusema ni namna gani tumeumia lakini ni kukuombea upumzike kwa amani. Mama ulitulea kama watoto wako wa kutuzaa pale Kibosho,ulitupenda na ukaweka upendo kati yatu kama familia moja. Kweli tunajivunia sana upendo,upole,ujasili,usafi na kujiamini uliotujengea mama unatusaidia sana katika maisha yetu,katika familia zetu na katika nyumba zetu, Ulikuwa mama mwema kwetu kwa wote tuliopita katika mikono yako.Tunakuombea mama upumzike kwa amani.R.I.P Mother Conso.
    Rosemary Makene

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli tumesikitika sana,hatuna hata namna ya kuelezea masikitiko yetu.Tunamwomba mwenyezi Mungu akupumzishe kwa amani katika makao ya Milele.''Raha ya Milele Umpe e Bwana na Mwanga wa Milele Umwangazie ,Apumzike kwa Amani -Amina''
    Martina Massawe

    ReplyDelete
  5. Jamani mama!!roho ziatuuma lakini hatuna jinsi,upumsike kwa amani mama,mama wetu wa upendo conso...tulikupenda mama lakini mwenyenzi mungu alikupenda zaidi...jina la bwana libarikiwe..pumzika kwa amani mama..
    Lillian Urasa sweden

    ReplyDelete
  6. Jamani Mother Conso wetu, tulikupenda ila Mungu kakupenda zaidi. Ulale kwa amani mama yetu mpendwa. Upendo wako kwetu hauna maelezo,malezi yako mema yametufanya nasi kuwa mama wema na wajasiri. Ulitupa misingi mizuri katika maisha yetu ambayo tutajivunia daima. Ulitulea kama watoto wako binafsi. Rest in peace Mother Consolata.

    Susan Mrango.

    ReplyDelete
  7. Nilifikiiri sr fidesta wa kifungilo.poleni watoto wakibosho maana I can't imagine to loose our mother too sr fidesta

    ReplyDelete
  8. Laura D. ShaoOctober 18, 2013

    Mother Consolata tutakumiss na kukumbuka daima, ulikuwa kioo cha maisha na ulitupa elimu bila ubaguzi tuitumie na iwe ufunguo wa Maisha. Aliyeyapokea maneno yako kwenye assembly point ameweza kuishi na kujiheshimu kufanikisha adhima ya maisha yake.. Hatutakusahau kamwe na usemi wako "mmenisikia vijana"... assembly dismiss. RIP Maza Conso. Laura Doris Shao

    ReplyDelete
  9. Wahenga wanasema nani kama mama hakuna basi Mother ulkuwa ni mama wa kipekee. Tulipokuwa katika mikono yako oooh tulideka tulipata maadili mazuri na hatimaye tulijengeka na kujua ni namna gani tunaishi katika jamii kama kioo cha maendeleo
    Mwenyezi akupe raha ya milele

    ReplyDelete
  10. Mama yetu mpendwa Consolata Shayo, ni huzuni isiyoelezeka kututoka tukiwa bado tunakupenda sana. Ulikuwa Kiongozi Jasiri na Mama Shujaa. Ulitupa misingi Imara tunayojivunia kama wamama shujaa wa Africa, asante kwa urithi wa malezi bora tunayoendelea kuwarithisha wanajamii wote.Tutakuenzi daima kwa vitendo kwa kuwa mifano bora na yakuigwa popote pale tutakapokuwa. Mungu akupe pumziko la amani na mwanga wa milele akuangazie mpendwa wetu Mother Consolata. Poleni sana wanafamilia na wana wa Kibosho girls' Sec School 1960s - todate.
    Cathy Mworia.

    ReplyDelete
  11. Kimwili umetuacha lakini maadili yako hayatatuacha kamwe.

    ReplyDelete
  12. Mama yetu mpendwa Consolata Shayo, ni huzuni isiyoelezeka kututoka tukiwa bado tunakupenda sana. Ulikuwa Kiongozi Jasiri na Mama Shujaa. Ulitupa misingi Imara tunayojivunia kama wamama shujaa wa Africa, asante kwa urithi wa malezi bora tunayoendelea kuwarithisha wanajamii wote.Tutakuenzi daima kwa vitendo kwa kuwa mifano bora na yakuigwa popote pale tutakapokuwa. Mungu akupe pumziko la amani na mwanga wa milele akuangazie mpendwa wetu Mother Consolata. Poleni sana wanafamilia na wana wa Kibosho girls' Sec School 1960s - todate.
    Cathy Mworia.

    ReplyDelete
  13. Tunakushukuru Mama kwa kutujenga, japo wakati ule tulikushangaa ulivyokuwa mkali lakini sasa tunatambua ulikuwa upendo wetu kwetu. Tunashukuru pia kutupa nafasi ya kukuhudumia na hata kukuona ulipoturuhusu kukuleta Dar kwa matibabu. Mama tulikupenda ila Mungu ameona unahitaji pumziko. Asante kwa yote. Pumzika kwa amani Mama, wanao umetupa yote tunaweza kusisimama.
    Xkibosho

    ReplyDelete
  14. Bibi Yangu Mpendwa ulinilea katika misingi yote ya kidini na malezi mazuri sina cha kukulipa na sitaweza kukulipa zaidi ya kukuombea tu Bibi yangu Mpendwa ukapumzike salama Bibi.
    Tunakukumbuka sana sisi wajukuu zako. Ukapumzike kwa Amani.

    ReplyDelete
  15. Mungu uweke moyo wa mpenzi mpendwa mama mahali pema. Namshukuru mungu kuwa miongoni mwa uangalizi wako. Ulijitolea asilimia 100 kutuangalia na kila ulolifanya uliku ukifanya kwa faida ya watoto wako. Kumbukumbu nyingi ninazo hasa ulipokuwa ukirudi safari , tukiona gali tunakimbilia tukipiga makelele" mama mama " siku inayofwata tunakua na assembly unatueleza kuhusu safali yako na kusema umefanikiwa nini kuhusu maendeleo ya shule . Umeacha Kumbukumbu ambayo itaendelea milele na milele. Mapumziko mema, Amen

    ReplyDelete
  16. Nashukuru kwa kwa huduma hii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...