Kwa masikitiko makubwa napenda kuufahamisha UMA kuwa utapeli alioutaja Ndugu Mpenda Haki upo na inawezekana kabisa umewaathiri wutumiaji wengine wa mitandao bila wenyewe kujua. Mimi nimepokea mpaka jana CV 4 za watu tofauti wakiomba kazi kwenye kampuni yangu. Kwanza niseme sina Kampuni ila naamini kabisa matapeli hawa wametumia email yangu kutangaza kazi, kama siyo hivyo basi wamefungua email inayofanana karibia kabisa na yangu..

Nilipopokea CV kwa mara ya kwanza nilifikiri  ni scam nika-delete. Nimepokea email zingine tatu toka kwa _Last Names Only: Mbasa, Msigwa and Jonathan jumla nne pamoja na ile ya kwanza. Jambo moja muhimu hapa Barua za kuomba kazi zinazo ambatanishwa na CV  zimeandikwa sawasawa kana kwamba zimeandikwa na mtu mmoja na  kubadilisha kile alichosomea na uzoefu. Sina uhakika kama mdau Mpenda
 
Haki alikua na maana ya utapeli wa aina hii au kuna mwingine
unaendelea. Kwa kifupi kabisa kama mtu akiona tangazo la kazi sehemu
likimtaka atume email kwenda sterling..()@yahoo.co.uk, tafadhali
usitume CV yako will just be deleted halafu ukae unahesabu umeomba
kazi kwenye Kampuni fulani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mimi nadhani email za hivyo zimeshafika 10 huwa na delete naona junk mail kumbe kuna utapeli ndani yake. Hii ni hatareeeeee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...