Bango maalum lililoandaliwa na Mtanzania kwa Watanzania katika hafla ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius  Kambarage  Nyerere maafuru kama  Mwalimu Nyerere Day iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Jumatatu Oktoba 14, 2013
 Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akiashiria uzinduzi wa uzinduzi wa kitabu  kilichopewa jina "Julius Nyerere African's Titan on a Global State: Perspective from Arusha to Obama"  kilichoandikwa kwa pamoja kati ya  Mwanazuoni  Maarufu Professa Ali Mazrui na   Professa Lindah Mhando. 
 Professa Ali Mazrui akionyesha kitabu kuhusu  Mwalimu Nyerere  ambacho yeye na Profesa  Lindah Mhando wamekiandika
 Naibu Katibu   Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Jan Elliasson ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Mwalimu Nyerere Day pembeni yake ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi. Chini ni sehemu ya umati uliohudhuria

Uwakilishi wa Kudumu wa  Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  kwa mara ya kwanza  umeadhimisha kwa namna ya pekee kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius  Kambarage  Nyerere maafuru kama  Mwalimu Nyerere Day. 
Hafla  hiyo  imefanyika siku ya  Jumatatu hapa  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa  na mgeni Rasmi alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw.  Jan Eliasson ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.  Hafla hiyo pia iliendana na  uzinduzi wa kitabu  kilichopewa jina "Julius Nyerere African's Titan on a Global State: Perspective from Arusha to Obama"  kilichoandikwa kwa pamoja kati ya  Mwanazuoni  Maarufu Professa Ali Mazrui na   Professa Lindah Mhando. 
Wageni mbalimbali wakiwamo mabalozi wanaoziwakilisha  nchi zao katika Umoja wa Mataifa walipata fursa ya kutoa salamu zao zilizosheheni  masuala makuu ambayo  Baba  wa  Taifa enzi za uhai wake aliyasema kwa nguvu zake zote,  masuala ambayo kwa mujibu wa  wazungumzaji hao   mengi kati yake yanaendelea  kutekelezwa au kuzungumziwa  hata  sasa katika  duru za kimataifa,  ni pamoja na  uhuru na utu wa mtu  mweusi, maendeleo shirikishi yakiwamo malengo ya maendeleo  ya millenia , kupiga vita umaskini, magonjwa na  matumzi ya  silaha  kali kama vile  silaha za nyuklia,  alikuwa mstari  wa mbele katika  kuhakikisha  nchini nyingi  hasa zile za  kusini mwa afrika zinapata uhuru wake na  vilevile alikuwa kiongozi aliyeona  mbali na aliyeweza kuwaunganisha siyo tu watanzania bali hata waaafrika wengine.


 Kwa  taswira zaidi  ya tukio hilo pamoja na  Salamu za Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na wazungumzaji wengine: 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...