Chemba ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo TCCIA imesherehekea miaka 25 ya kuanzishwa kwake kwa kufanya kongamano kubwa lililowaunganisha sekta binafsi na serikali.Mamia ya wafanya biashara na taasisi za serikali wamejuimuika pamoja kujadiliana masuala mbalimbali na kero zinazowakumba wafanya biashara.
Waziri Wa Viwanda na Biashara Mhe. Dr. Abdallah Kigoda(Mb) akiongea na wafanyabiashara katika kongamano hilo.
Kogamano hili lilijadili Kero na mazingira ya kufanya biashara Tanzania na namna yanavyowezesha biashara kuwa na tija kwa mfanyabiashara na serikali kwa ujumla katika kukuza uchumi wa Taifa. Wadau kutoka sekta mbalimbali kutoka taasisi za utafiti, chuo kikiuu cha Dar es Salaam, wafanyabiashara na wadau wengine kutoka taasisi za sekta binafsi walishiriki kwa kutoa mada fupi za kuchokoza mjadala.
Baadhi ya Washiriki wakifuatilia kwa makini Mada mbali mbali ambazo ziliwasilishwa wakati wa Mdahalo huo.
Mada zilizojadiliwa ni pamoja na;-
1. Kurejeshwa kwa ada za leseni za biashara na madhara yake kwa wafanya biashara.
2. Madhara ya kanuni na sheria nyingi zihusuzo biashara na athari zake katika mazingira ya ufanyaji wa biashara
3. Madhara ya machine za ukusanyaji kodi kwa jumuhia ya wafanyabiashara”
4. Madhara ya masamaha wa ushuru kwa baadhi ya biashara kwa wafanyabiashara wa ndani ya nchi”
5. Madhara ya uwepo wa mizani nyingi za barabarani pamoja na vizuizi vya polisi na
6. Changamoto zinazowakabili wanawake wajasiriamali wanaofanya biashara za mipakani iliyotolewa na
7. Sera ya kulinda viwanda vya ndani na madhara yake kwa wawekezaji wa ndani
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...