The World Islamic Economic Forum (WIFE) imeanza kikao chake cha tisa jijini London nchini Uingereza Jumanne 29/10/2013 na kuendelea hadi 31/10/2013. Zaidi ya wajasiriamali 1,000 kutoka zaidi ya nchi 100 na viongozi zaidi ya 15 wa mataifa mbambali watahudhuria. Hii ni mara ya kwanza kwa mkutano huo kufanyika ktk nchi isiyokua ya ki-Islam.
Akizungumza kuhusiana na mkutano huo Waziri wa uchumi wa Uingereza Mh. George Osborne alisema ‘huu ni mfano mzuri wa nafasi ya Uingereza kama kituo muhimu cha uchumi wa dunia'. Aliongeza kua uchumi unaofuata maadili ya ki-Islam unakua kwa asilimia 50 na una kila sababu ya kukua zaidi.
Pamoja na mambo mengine yaliyojadiliwa kuna vitu viwili ambavyo vilichukua umuhimu wa aina yake navyo ni kama alivyoeleza Mh. Huyo kuwa “Our ambition is clear: to make Britain the first sovereign to issue an Islamic bond outside the Islamic world,” British finance minister George Osborne wrote in a column in the Financial Times on Tuesday’.
Kitu kingine alizungumzia swala zima la kuanzisha Index inayofuata maadili ya ki-Islam alisema ‘The London Stock Exchange also announced plans to launch an Islamic index which would identify companies which are filtered according to Islamic principles, which work in much the same way as socially responsible screens.
Kwa upande mwingine ‘Prime Minister David Cameron made a bid to position London as a leading hub for Islamic finance on Tuesday.
Tutaendelea kuwaletea matukio ya mkutano huo na kuwafahamisha kinachoendelea. Kwa wakazi wa Uingereza na maeneno ya jirani wanaweza kuhudhuria mkutano huo unaofanyika Excel ambapo kiingilio ni £300 kwa mtu mmoja.
Kwa maelezo zaidi kuhusu benki zinazofuata maadili ya ki-Islam wasiliana na http://ijuebankyakiislam.blogspot.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...