Balozi Tanzania Nchini Zambia,Mh. Ggace Mujuma (mwenye nguo za vitenge) akikabidhi msaada wa chakula kwa uongozi wa hospitali kuu ya Taifa ya Nchini Zambai (UTH) iliopo jijini Lusaka,msaada huo umetolewa na Ubalozi huo kwa kushirikiana na Jamii ya watanzania waishio Lusaka Zambia wakiadhimisha kumbukumbu ya kifo cha baba wa Taifa Mwl Nyerere.
mmoja wa wahitaji akiwa amelala chini ikiwa ni ishara ya Furaha na shukrani kwa msaada wa chakula walioupata kutoka kwa jumuiya ya watanzania waishio Lusaka Zambia walioshirikiana na Ubalozi kutoa msaada huo.mama Huyo alionyesha heshima ya Kiwango cha juu iliyopo kwenye Baadhi ya mila Za kiafrika wakati wa matukio mbalimbali ya kijamii ikiwa ni pamoja na kutoa shukrani kwa jambo jema.
Baadhi ya wana jumuiya ya watanzania waishio Lusaka Zambia wakiwa pamoja na Balozi Grace MUJUMA na wafanyakazi wenzake wa Ubalozi bw jeswald Majuva na bw huddy Kiangi katika tukio la utoaji msaada wa chakula kwenye hospitali kuu ya ZAMBIA iliyoko Lusaka. Msaada huo wa chakula kwa wagonjwa waliolazwa kwenye hospitali hiyo umetolewa ikiwa ni kumuenzi baba wa Taifa kwa mapenzi yake kwa Jamii ya watu wenye shiva na wale wanyonge.
Ubalozi wa Tanzania Lusaka Zambia kwa kushirikiana na jumuiya ya watanzania waishio Lusaka Zambia hawakuishia kutoa msaada wa chakula kwenye hospitali kuu nchini Zambia ya university teaching hospital pekee Bali walikwenda na kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha TAZA kilichopo Barabara ya chilimbulu jijini Lusaka kutoa msaada huo.matukio haya yamefanyika kwa pamoja ikiwa ni maadhimisho ya miaka 14 tangu alipofariki baba wa Taifa Mwl JK Nyerere na hivyo haja ya kumuenzi kwa matendo yake kwa watu wanyonge ilikuwa ya muhimu kuzikumbuka Jamii zenye mahitaji muhimu.itakumbukwa kuwa baba wa Taifa alipendwa sana na wananchi wa ZAMBIA hususani kwa jitihada Zake za ukombozi wa bara la afrika na utetezi wake kwa watu wanyonge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...