Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O.
Kombani (Mb) akiongea ofisini kwake katika hafla fupi ya kuipongeza timu
ya mpira wa Pete ya Utumishi mapema leo.
Mwenyekiti wa Klabu ya michezo ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma Bw.Lumuli Mtaki akisoma ripoti kuhusu klabu yake ya Utumishi
wakati wa hafla fupi ya ya kuipongeza timu ya mpira wa Pete ya Utumishi
iliyofanyika ofisini hapo mapema leo.
Watumishi na Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
wakimsikiliza Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Utumishi Mh.Celina O. Kombani
(Mb) wakati wa hafla fupi ya kuipongeza timu ya mpira wa Pete ya Utumishi
iliyofanyika ofisini hapo mapema leo.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O.
Kombani (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Mpira wa Pete ya
Utumishi mara baada ya hafla fupi ya ya kuipongeza timu hiyo iliyofanyika
ofisini kwake mapema leo.Wengine mstari mbele ni Kapteni wa timu hiyo
Bi.Elizabeth Fussi (mwenye kikombe), Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB
Mkwizu , na kushoto kabisa ni Mwalimu wa timu Bw Mathew Kambona na Katibu
Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (kushoto kwake).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...