Na John Nditi
Wahamiaji haramu raia wa Ethiopia ambao walikamatwa Oktoba 12, mwaka huu eneo la Chamwino ,Manispaa ya Morogoro katika barabara kuu ya Morogoro – Iringa wakiwa ndani ya lori lililosheheni mzigo wa chokaa na kaufunikiwa na turubai lililokuwa likitokaTanga kwenda Congo ( DRC) , wamefikishwa mahakamani leo Oktoba 15, Mwaka huu na kusomewa kwa mara ya kwanza. Kesi yao ya kuingia nchini bila kuwa na vibali wala hati ya kusafiria zinazotolewa na Serikali ya Tanzania imeahirishwa hadi Oktoba 28, mwaka huu.
Wahamiaji haramu hao wakipata kifungua kinywa Mahakamani Morogoro
Chai kwanza, mashitaka baadaye
Lori lililokamatwa kiliwa limewababe na kuwafunika na turubai raia 16 wa Ethiopia wakisafirishwa kwenda nchi za kusini mwa afrika , Oktoba 12, mwaka huu, likiwa chini ya ulinzi
Maofisa wa Uhamiaji wakishikilia Dereva Ally Muhamango (45) mkazi wa Temeke, Dar ambaye ni dereva wa Lori hilo lililobeba chokaa na wahamiaji haramu 16 wa kutoka Ethiopia.


kwa style hii na mimi naomba mnikamate maana nina miezi kibao sijala mkate,kifungua kinywa changu ni uji wa chumvi
ReplyDeletemwenye kesi hapo ni dereva na mmiliki wa gari maana hao ndo wamechukua fwedha kuwasafirisha..hao mnawaonea tuu!
ReplyDeletemmiliki wa gari anaweza asiwe anajua lolote kuhusu hilo labda kama ni muhimu kumhukumu kwa sababu tu anamiliki gari na wewe huna.
ReplyDeleteni vema pia itafutwe chanzo kwa nini wahamiaji haramu, huenda ni tatzo la kiufundi!""ila wabongo kwa kupenda pesa mtu anaweza hata kuuza wazazi wake!!! nashangaa nchi yetu ni maskin!!
ReplyDeleteKama hawajafanya kosa lolote warudishwe tu kwao. Watz hatuna bifu lolote na wahabeshi. Ila dereva akomaliwe kimtindo
ReplyDelete