Muonekano wa maandamano katika jiji la Arusha jana ikiwa ni tamasha la Arusha Festival lenye nia ya kumuhenzi baba wa Taifa Mwl.Julius Kambarage Nyerere lililofanyika katika uwanja wa General trye,waandaaji nikampuni ya  Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5 Arusha wakishirikiana  na  Kibo Palace Hotel,Pepsi,KK security,Radio 5,Shed and Sons,Shining Stars,DSTV na Trinity.
  Wanafunzi walioshiriki katika Tamasha hilo wakiwa wamebeba bango linaloelezea Arusha Festive huku pikipiki,tarumbeta zikipamba siku hii katika eneo la Mnara wa saa jijini Arusha wakiwa wanaelekea katika uwanja wa General tyre.
Maandamano hayo yalipambwa na  farasi wawili waliokuwa kivutio kikubwa sana kwa wakazi wa jiji la Arusha na Viunga vyake huku magari,pikipiki,wanafunzi pamoja na wadau mbalimbali walishiriki katika Tamasha hilo
 Vicky Mwakoyo ambaye ni Creative Meneja wa kampuni ya  Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5 Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na Sarah Keiya Meneja masoko wa kampuni katika uwanja wa General tyre
Wadau wa Tamasha hilo wakishoo love katika uwanja wa General trye huku michezo mbalimbali,ngoma za asili zikichukua nafasi yake katika sherehe za kumuenzi Baba wa Taifa,waandaaji nikampuni ya  Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5 Arusha wakishirikiana  na  Kibo Palace Hotel,Pepsi,KK security,Radio 5,Shed and Sons,Shining Stars,DSTV na Trinity.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. PAZIA HALINA MACHO......HAO NI NGAMIA SIO FARASI!!!!!

    ReplyDelete
  2. huyu mwandishi/ mleta habari lazima atakuwa ni mtoto mdogo, kwanza anaogopa wanyama ndio maana picha imepigwa wanyama wanaonekana kwa mbali, pili hawajui farasi wala ngamia. THATHAAA!! MTOTO MZURIII!!!! HAO NI NGAMIA THIO FARATHIII!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...